'Historia leo imeandikishwa Afrika Mashariki,'Raila ampongeza Suluhu baada ya kuapishwa

Muhtasari
  • Raila ampongeza Suluhu baada ya kuapishwa
  • Kinara huyo alisema kwamba anamuombea rais huyo mpya wa Tanzania mafanikio katika uongozi wake

KInara wa ODM Raila Odinga amempongeza Samia Suluhu baada ya kuapishwa na kuwa rais wajamuhuri ya Tanzania kufuatia kifo chake Pombe Magufuli.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter Raila alisema kwamba historia imeandikishwa Afrika Mashariki.

Kinara huyo alisema kwamba anamuombea rais huyo mpya wa Tanzania mafanikio katika uongozi wake.

"Historia leo imeandikishwa Afrika Mashariki.Hongera @SuluhuSamia kwa kuchukua hatamu kama rais wa kwanza wa kike wa Tanzania

Mimi na Mama @IdaOdinga tunakuombea mafinikio katika jukumu lililo mbele yako la kuwaongoza watu wako na kuimarisha uhusiano baina ya mataifa yetu," Aliandika Raila.

Suluhu aliapishwa siku ya Ijumaa, huku akiwa rais wa sita wa nchi ya Tanzania na mwanamke wa kwanza kuwa rais Afrika.

Rais huyo mpya wa Tanzania amekuwa naibu rais tangu mwaka wa 2015.