Nataka kusikia vile huwa mnasikia mkilipiwa gharama na mwanamume-Akothee

Muhtasari
  • Akothee afichua anachotaka siku ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa
akoth stylish 1 (1)
akoth stylish 1 (1)

Afrika mashariki nani kwa kweli hamfahamu manii Akothee?msanii huyo ni mwenye bidii katika kazi yake ya usanii.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alitangaza mpango wake wa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Akothee alisema kwamba siku hiyo anataka kulipiwa gharama zote na mwanamume na kusiki vile wanawake wengine husikia wakilipiwa gharama na wanaume wao.

Pia alifichua kwamba ni jambo ambalo hajakuwa akifanyiwa kwa miaka sasa baada ya baba ya watoto wake kumuacha.

"Nataka kujihisi kama msichana, siku ya kusheherekea siku yangu ya kuzaliwa inakaribia unafikiria aje mtu  kunilipia hoteli hii tangu tarehe 5 hadi 12

Nataka kuhisi vile mnahisi mkilipiwa gharama na mwanamume,sijahisi hivyo tangu Papa Oyoo aniache, nimechoka kujilipia gharama na kujinunulia zawadi," Aliandika Akothee.