'Yuko sawa lakini sio kabisa,'Caro Radull amtembelea Conjestina afichua anavyoendelea

Muhtasari
  • Mwanahabari wa spoti Carol Radull kwa mara nyingine amemtembelea mwanaspoti wa michezo ya masumbwi Conjestina ili kumjulia hali baada ya kuenda 'Rehab'
  • Radull ambaye alimtembelea Conjestina alidai kwamba anaendelea vyema lakini sio vyema kabisa
Carol-Radull-sports-696x418
Carol-Radull-sports-696x418

Mwanahabari wa spoti Carol Radull kwa mara nyingine amemtembelea mwanaspoti wa michezo ya masumbwi Conjestina ili kumjulia hali baada ya kuenda 'Rehab'.

Hali hiyo ya maisha ya Conjestina ilianza kubadilika Oktoba 2018, baada ya video yake kuibuka akidai kutengwa wakati anakabiliana na maradhi ya akili.

Baada ya miezi kadhaa ya matibabu, Congestina alionyesha kupiga hatua na kuwa kwenye safari ya kupata nafuu kikamilifu.

 

Radull ambaye alimtembelea Conjestina alidai kwamba anaendelea vyema lakini sio vyema kabisa.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Radull aliandika haya,

 "Hayuko mahali alipokuwa Julai mwaka jana lakini hayuko mahali ambapo nilitarajia angekuwa wakati huu.

Conjestina yuko sawa lakini sio sawa kabisa, Bado hana la kufanya baada ya ahadi bandia za "Baraza la Mashujaa"  ahadi na sio juu ya dawa zinazohitajika. Lakini tunajua hii ni safari. Mungu akubariki kila wakati rafiki yangu  🙏🏽 #AlutaContinua #ForTheLoveofTheGame," Aliandika Radull.

Mashabiki walipendezwa na hatua yake Carol Radull ya kumsaidia guli huyo.