Hapana tambua corona!Tazama jinsi Eric Omondi na Betty Kyallo walivyopokelewa na mashabiki Kisumu

Muhtasari
  • Wanamitandao wazua mdahalo baada ya Eric Omondi kupakia video hii

Wakenya wamezua mdahalo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuona jinsi mashabiki walikusanyika kwa pamoja na kumpokea mchekeshaji Eric Omondi na mtangazaji Betty Kyallo Kisumu.

Wengi wa wanamitando walishindwa kwani hamna corona kaunti ya Kisumu kwani wengi wao hawakuwa wamevalia barakoa wala kutangamana kwa mita moja.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram wa mchekeshaji Eric Omondi alipakia video ambayo ilionyesha jinsi walipokelewa na mashabiki huku bila ya kufuata kanuni za wizara ya afya ili kuthibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

Baada ya kupakia video hiyo aliandika ujumbe ufuatao;

"Nilimpeleka Betty Kyallo Kisumu mahali nilizaliwa na kulelewa, na wakasema iko saawa," Aliandika Omondi.

Wawili hao walianzisha kipindi chao kwenye runinga ya KTN.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

scottsbarnes: No face mask...you guys are not serious thou

prince._jere: Bt ingekua Ruto mgesema anafanya mkutano2h10 likesReply

tallman_kenya: So no corona 🤔😂

lylyane_fletcher: Hakuna covid😢😢

hon.ankobob: Kindly adhere to covid 19 rules

verahnyandieka: Social distancing 😒 😷

Hii hapa video iliyozua mdahalo mitandaoni