'Nilikuwa natumia elfu 50, kila siku kwa wanawake tofauti,'Jamal Roho Safi jinsi Amber Ray alimbadilisha

Muhtasari
  • Jimal Roho safi alifahamika sana baada ya kumuoa mwanasosholaiti Amber Ray mapema mwaka huu

Jimal Roho safi alifahamika sana baada ya kumuoa mwanasosholaiti Amber Ray mapema mwaka huu.

Akiwa kwenye mahojiano Jimal alifichua kwamba alilelewa kaunti ya Kajiado, huku baada ya kumaliza shule akaanza kufanya kazi ya makanga.

"Nina matatu zaidi ya elfi 100, nilianza kufanya kazi ya makanga baada ya kumaliza shule, nilikaa hivi nikasema kwamba siwezi fanya kazi hiyo miaka yangu yote," Alisema Jimal.

 

Kulingana na Jimal alimuoa Amber Ray mwaka huu baada ya wawili hao kuwa marafiki kwa miaka 5.

Pia mwanabiashara huyo alifichua kwamba  Amber Ray alibadilisha maisha yake, kutoka kuwa mtu mbaya.

Alisema kwamba alikuwa anatumia elfu 50, kila siku kwa wanawake tofauti, aimsifia Amber kwa kusema kwamba ni mwanamke ambaye ni mnyenyekevu, na ndio maana aliamua kumuoa.

"Amber ni mmoja wa wanawake ambao ni mwema hangejua kwamba angekuwa mke wa pili, pia mke wangu wa kwanza ni pole sana hana roho ngumu nilimwambia kuhusu Amber tukakosa kuongeleshana kwa wiki moja," Alieongea Jimal.

Hii hapa video ya mahojiano hayo;

#BongaNaJalas https://jalangotv.com/ To Subscribe To PichaClear Youtube Channel Click this link https://www.youtube.com/pichaclearfilms