Ben Pol hatimaye azungumzia talaka yake na Anerlisa Muigai

Muhtasari
  • Ben Pol azungumzia talaka yake na Anerlisa Muigai
  • Kupitia taarifa rasmi Ben Pol alizungumzia talaka na kusema kwamba wanataka kupewa nafasi hasa wakati huu ambao wanapitia changamoto
Anerlisa-and-Ben-Pol-in-each-others-arms-696x527
Anerlisa-and-Ben-Pol-in-each-others-arms-696x527

Baada ya Anerlisa Muigai kuthibitisha kwamba alitia saini karatasi za talaka, hatimaye mumewe msanii Ben POl pia naye amethibitisha kwamba ni jambo ambalo liko kwa korti.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram wake Anerlisa aliwaambia mashabiki kwamba alitia saini kile kilichohitajika na kwamba hataki kuhusishwa na mtu yeyote.

Kupitia taarifa rasmi Ben Pol alizungumzia talaka na kusema kwamba wanataka kupewa nafasi hasa wakati huu ambao wanapitia changamoto.

 
 

Pia alishukuru kila mtu ambaye amekuwa akimuunga mkono na kumjulia hali.

"Kwa wakati huu Ben Pol anataka kusema kwamba kesi ya talaka inaendelea kortini lakini haijakamilika

Kesi hii ni ya siri sana, na hangetaka kuzungumza chochote kwa ajili ya heshima kwa pande zote mbili," Ilisoma taarifa.

Katika taarifa yake hakumtaja mkewe Anerlisa, bali aliomba nafasi, huku usimamizi wake ukisema,

"Anaomba kupewa nafasi,na faragha pamoja na familia yake hasa wakati huu wanapitia changamoto, anawashukuru wote ambao wameelewa

Na anchukua fursa hii kushukuru failia, marafiki na mashabiki kwa kumpa usaidizi,"

Wawili hao walifunga ndoa mwaka jana katika harusi ya kifahari na ya kipekee huko Tanzania.