Mke wangu aliniacha baada ya kumwambia twende mashambani-Asimulia mwanamume

Muhtasari
  • Katika bustani la Massawe Japanni mwanamume mmoja alifichua kisa cha kuachana na mke wake

Ukiamua kuingia kwenye ndoa lazima ukubali kile mume wako anakuambia kwa maana katika desturi ya waafrika mwanamume ndio kichwa cha familia na mwanamke shingo.

Katika bustani la Massawe Japanni mwanamume mmoja alifichua kisa cha kuachana na mke wake.

Mwanamume huyo alifichua kuwa kabla ya kuachana na mke wake walikuwa wamebarikiwa na mtoto mmoja na kuwa mkewe alikuwa haambiliki.

Mwanamume huyo alikuwa anachangia mada kwanini wakati huu au karne hii ya sasa wanaume wengi hawaoi na wanawake hawaolewi.

Huu hapa usimulizi wake;

"Mimi nilikuwa na bibi, lakini alikuwa kichwa ngumu sana pia alikuwa haambiliki licha yake kuwa mke wangu, siku moja niliamka na nikamwambia  nataka twende mashambni Kakamega kwa maana tulikuwa tunaishi Mombasa

Siku hiyo ndio aliniacha, na kutoka kwenye ndoa yetu, kwa hvyo wanawake wengi hawataki kuolewa wala kuwasikiza waume zao," Alieleza mwanamume huyo.

Je kwanini wanaume na wanawake wa karne hii hawtaki kuingia kwa ndoa?