'Waambie kitu unachoamini ni kondomu,'Doreen awashauri wagonjwa wa ukimwi kunywa dawa za ARV's

Muhtasari
  • Doreen awashauri wagonjwa wa ukimwi kunywa dawa za ARV's

Mwanaharakati wa wagonjwa wanaougua virusi vya ukimwi Doreen Moraa Moracha kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewashauri wagonjwa hao waweze kunywa dawa zao.

Awali akiwa kwenye mahojiano Moraa alifichua kwamba madaktari walidai kwamba ataaga dunia kabla ya kuhitimu miaka 12.

Lakini hawakukosea waliposema alipangalo Mungu hakuna wa kulipangua.

Pia aliwashauri wagonjwa hao wanapaswa kunwa dawa za ARV's licha ya kukataliwa katika jamii zao.

"Fikiria kukataa kuchumywa ARV zako kwa sababu ya kukataliwa basi kutambua nimekuwa kwenye ARV kwa miaka 16 iliyopita πŸ‘―β™€οΈ "Kunywa" ARV yako na kustawi kwa kuwa wanadamu wangu wasio na HIV wanakaa  hivyo kama kwamba ikiwa mtu anauliza "mpenzi huniamini"

Waambie kwamba kitu ambacho unaamini ni kondomu za trust," Aliandika Doreen.

Doreen amekuwa katika mstariwa mbele akiwatetea wagonjwa wa ukimwi na kutaka wapate haki zao.