'Mitandao ya kijamii ni nafasi mbaya sana kwa watoto,'Risper Faith afichua kwanini hampakii mwanawe mitandaoni

Muhtasari
  • Risper Faith afichua kwanini hampakii mwanawe mitandaoni
Risper Faith and Brian Muiruri
Risper Faith and Brian Muiruri

Mwanasosholaiti Risper Faith, kwa mara ya kwanza ameweka wazi na kuzungumzia sababu yake ya kutopakia mwanawe mitandaoni.

Kulingana na Risper mitandao ya kijamii ni nafasi mbaya sana kwa watoto, kwani kila mtu huwa na maoni yake.

Akiwa kwenye mahojiano na bonga na Jalas, mwanasosholaiti huyo alisema kwamba ni uamuzi walifanya akiwa na mumewe, ili kumlinda mtoto wao kutoka kwa kejeli nyingi.

Ndio sio wanamitandao wote ambao wana utu kwani tumeshuudia, ata watu maarufu wakishikwa na msongo wa mawazo kwa ajili ya kejeli nyingi kutoka kwa wanamitandao.

 

"Mitandao ya kijamii ni nafasi mbaya sana kwa watoto. Nilichagua kutompakia mwanagu mitandaoni

 Unaweza kufikiria mtoto wako anaonekana kuwa mkamilifu lakini mtu mwingine atatafuta makosa, Ooh Hakukai Ooh Hakai Brian.

Niliamua kumchagua kama anataka kuwa kwenye mitandao ya kijamii  au la," Alisema Risper.

Risper na Brian walibarikiwa na  mtoto wao Desemba 2018, baada ya wawili hao kufunga pingu za maisha Februari mwaka huo huo.

Pia alifichua kwamba alifanya tendo la ndoa na umewe, siku ya kwanza kukutana naye kwani alikuwa ametoka nchi za nje, na hakuwa anataka kumpoteza.

Risper akiwa kwenye mahojiano alisema kwamba hajawahiogopa kwamba mumewe anaweza chukuliwa na wanawake wengine ambao wanamtumia jumbe.