'Nampeza sana hasa wakati kama huu,'Msanii Moji Shortbabaa asema haya kuhusu mama yake

Muhtasari
  • Hatimaye kikundi hicho, kilikikwisha huku kila mmoja akianza kufanya kazi ki vyake
  • Moji aliendelea kutoa kibao kimoja baada ya kingine, huku vibao vyake vikipendwa sana na wanamitandao na mashabiki wake
Moji Shortbaba
Image: Hisani

Moji Shortbaba ni msanii wa Injili ya Kenya, mwandishi wa nyimbo, na muigizaji. alifahamika sana kupitia kwa kikundi kinachofahamika kama "Kelele Takatifu" ambacho kilichukua wimbi la injili kwa ngazi nyingine.

Hatimaye kikundi hicho, kilikikwisha huku kila mmoja akianza kufanya kazi ki vyake.

Moji aliendelea kutoa kibao kimoja baada ya kingine, huku vibao vyake vikipendwa sana na wanamitandao na mashabiki wake.

Kupitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, alitamani sana mama yake angekuwa hai ili kushuhudia msanii huyo akiadhimisha mwaka mwingine.

Moji aliandika ujumbe wa kihisia, na ujumbe huo ni kama vile ufuatao;

"Furaha ya kuzaliwa kwangu! 🎉 Kumshukuru Mungu kwa mwaka mwingine! Natamani mama angekuwa hapa kumwona mvulana wake mdogo amekuwa mzima, nampeza zaidi siku kama hizi! Asante Yesu kwa uaminifu wako kila mwaka na kila siku!" Aliandika Moji.