Seneta Millicent Omanga amsifu Terence Creative asema anahitaji 'Kemikal'

Muhtasari
  • Utapeli wa fedha umekuwa  mjadala mkubwa unaoendelea katika wiki chache zilizopita
  • Kashfa na tapeli zimegonga vichwa vya habari mitaani
omanga
omanga

Utapeli wa fedha umekuwa  mjadala mkubwa unaoendelea katika wiki chache zilizopita.

Kashfa na tapeli zimegonga vichwa vya habari mitaani.

Mchekeshaji Terence kupitia habari hizo na ubunifu ameamua kuwafurahisha mashabiki wake kupitia kwa tukio hilo.

Amewashirikisha video yake kuwashawishi familia zenye wasio na hatia ambao wanatamani sana kufanya mamilioni ya fedha kwa kuzunguka tu au tu kulala juu ya vitanda vyao.

Baada ya muda familia hio zinajuta na kulia baada ya kupata hasara kubwa.

Video yake imekuwa ikienea kwenye mitandao ya kijamii na YouTube. Alisema kuwa ni video inayotazamwa  zaidi kwa siku.

Video hii ilivutia tahadhari ya mwanasiasa maarufu seneya Millicent Omanga.

Hata hivyo kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook alishiriki picha yaTerrence na kuonyesha jinsi alivyoshukuru kuhusu maudhui yake.

"Ngakubali Terence creative ngakuwa talented sanaa. Ngataka ngauzia mimi kemikal pia," Aliandika Millicent.

Hizi hapa baadhi ya hisia za wanamitandao;

Julius Jumah Mlavidavi ยท:  Kemikal ngatengeza pesa ya kampeni nga mama kanairo. Ngapewa medizin

Apple Santa Sonny: Sasa kenye imebaki ni jayden na matiangi kusema nga nga nga iwekwe kwa sereebas.....si sisi wote ni wendawazimu๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Khan Sean: Ngakunywa kemikal ngakufa ngu๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…

Derrick Omondi: Mimi ngatafuta wewe Niko na Kemikal yenye wewe ngapenda saana