'Kwa nini uandike kitu kama hicho,' King Kaka kwa wanaoeneza uvumi kuwa amebakisha mwezi mmoja wa kuishi

Muhtasari
  • King Kaka akemea uvumi kwamba amebakisha mwezi mmoja wa kuishi
King Kaka
Image: Hisani

Ni wazi kuwa rapa maarufu King Kaka alikuwa anaugua, kwa kiezi tatu, huku habari za ugonjwa wake akiwafahamisha mashabiki wake.

Mapema mwezi uliopita rapa huyo alifichua kwamba vipimo vibaya na madawa ambayo alipatiwa na daktari katika hospitali moja nchini yalimsababishia madhara mabaya mwilini.

Kaka alieleza kwamba aliugua maradhi ambayo yalimfanya apoteze kilo 33, apoteze hisia ya ladha, kiuno chake kupungua kati ya dalili zingine.

"Haijalishi ushindi ni mdogo kiasi gani bado ni ushindi tu uliangalia uzito wangu na nimepata kilo 6. Kupotezakilo zote hizo haikuwa utani na sasa kuona faida ni motisha kubwa na baraka. Asante kila mtu ambaye alisali Twendelee ubarikiwe. " Mwanamuziki huyo alitangaza kupitia mtandao wa Instagram wiki iliyopita.

Ingawa King Kaka amepiga hatua kiasi katika safari yake ya kupata afueni kikamilifu, ni dhahiri kuwa bado hisia yake ya ladha haijarejea kikamilifu.

Asubuhi ya Jumatano King Kaka alisuta vikali mwanablogu ambaye alikuwa amechapisha habari za uongo eti alikuwa amebakisha muda mfupi duniani.

Picha ambayo alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram ilionyesha habari zilizodai kuwa alikuwa ameaga Wakenya kwaheri kwa kuwa daktair alikuwa amemuarifu kuwa amebakisha mwezi mmoja wa kuishi.

"Shida ya blogs huwa nini? Mbona uandike kitu kama hiyo? Hata hivyo ata adui ambaye ako na shida ya kulala halali kweli." Kaka aliandika chini ya ujumbe huo.

Wanamitandao wengi walijumuika kumkashifu mwanablogu aliyekuwa ameandika habari hizo za uongo.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

wanjikustephens: They need to be sued to be an example

ykeebenda: 🙏🏻You will be fine brother ..beliv that

shannel_uk: May you live 40000000000000000 years to come

janetmuhoro7: Enemies of progress you will and testify the Goodness of Our God 🙏 live long King 😮

anyangoakinyi: 😢😢washidwee shetani hao!!