Muziki wetu utaenda mbali tukiacha chuki,'Rayvanny azungumzia ukosefu wa umoja wa wasanii

Muhtasari
  • Rayvanny azungumzia ukosefu wa umoja wa wasanii
rayvanny
rayvanny

Diamond na Harmonize wamo Marekani kwa ziara ya kimziki, na baadhi ya watanzani wamekuwa wakimsifu Diamond huku wengine wakimkejeli Harmonize.

Huku msanii Rayvanny akizungumzia hayo alisema kwamba usanii wao unawea enda mbali wasanii wakiacha chuki.

Ni kawaida Harmonize na Diamond hawajakuwa wakiskizana, hii ni baada ya Harmonize kutoka katika lebo ya WCB.

Wasanii kutoka Nigeria wamekuwa wakishikana mkono baada kuenda Marekani.

"Muziki wetu unapoenda sio pabaya na utafika mbali tukiacha chuki na kuumia unapoona mwenzako anafanya vizuri ...

Wenzetu mmoja wao akifanya vizuri wote wanamsapoti basi nasisi tufanye kama wenzetu ili tufike mbali .....

NASAPOTI KILA ANAEFANYA VIZURI SABABU MMOJA AKIFANIKIWA IMEFANIKIWA INDUSTRY YETU LETS GO GLOBAL 🌏🌍🌏🌍πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯🌟🌟," Aliandika Rayvanny.

Tumeshuhudia na na kuona jinsi wasanii kutoka nchi tofauti wamekuwa wakishambuliana kwenye mitandao ya kijamii.