'Moyo wangu una maumivu,'Mpenzi wake nduguye Baha amkumbuka mwanawe

Muhtasari
  • Muigizaji wa zamani wa Makutano Junction Mungai Mbaya na mpenzi wake Mo Aisha wanaonekana kuwa bado wana kumbukumbu za marehemu mtoto wao

Miezi mitano haswa tangu kufariki kwa mtoto wao wa mwezi mmoja; Muigizaji wa zamani wa Makutano Junction Mungai Mbaya na mpenzi wake Mo Aisha wanaonekana kuwa bado wana kumbukumbu za marehemu mtoto wao mchanga ambaye kwa hakika alikuwa na nafasi ya pekee mioyoni mwao kwa muda mfupi.

Akitumia mtandao wake wa Instagram, Aisha ambaye pia ni shemeji wa mwigizaji wa zamani wa Machachari Baha, alifichua waziwazi jinsi kifo cha mwanawe mchanga bado kinaibua kumbukumbu na mihemko ndani yake.

"Moyo wangu una maumivu. Maumivu ambayo sielewi. Natamani ningeweza lakini sifanyi. Moyo wangu unauma kwa ajili yako Lyric

Siku haipiti bila mimi kukufikiria. Ya kile ambacho kingeweza kuwa. Ungekuwa mvulana mkubwa kwa sasa

Tungeanza kumwachisha ziwa, jambo ambalo mimi na Baba yako tulitazamia. Maisha yetu si ya kawaida tena na hayatakuwa kamwe

Tulipoteza sehemu kubwa sana ya maisha yetu, WEWE, mzaliwa wetu wa kwanza. Angalau naweza kusema nilibahatika kuwa mama wa mtoto wa ajabu sana

Najua umeenda lakini sijisikii hivyo. Sijui kama sio mimi sijashughulikia kifo chako au ninahisi uwepo wako

Kwa vyovyote vile naamini uko hapa na malaika wako mlezi. 🥺 Siwezi kusubiri kukutana nawe tena na kukuona Lyric. Heri ya kuzaliwa kwa  mwezi wa 5❤️ MAMA ANAKUPENDA SANA❤️," Aliandika Mo.

Zaidi ya hayo, Aisha pia alishiriki taarifa fupi kuhusu hadithi yake ambayo ilionyesha wazi maumivu yake yasiyoelezeka kuhusiana na maadhimisho hayo.

Lyric alikuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa kwa wanandoa hao mashuhuri lakini baadaye aliambukizwa na maambukizi mwezi mmoja tu baada ya kuzaliwa kwake.

Kulingana na maungamo kadhaa kutoka kwa Aisha, hii imekuwa moja ya nyakati zake zisizosahaulika.