Mashuhuri maskini!Mtumba Man afichua alivyotaka kujitoa uhai baada ya kuwa maarufu

Muhtasari
  • Mtumba Man afichua alivyotaka kujitoa uhai baada ya kuwa maarufu
Mutuba man
Image: Hisani

Tunapozungumzia Mtumba Man, wengi wanamfahamu kama mwanamume ambaye anauza mitumba akiwa anaimba na kuvalia mavazi ya wanawake.

Je uewahi jiuliza kwa nini watu mashuhuri au vijana mashuhuri ujitoa uhai au kupatwa na msongo wa mawazo licha yao kuwa maarufu nchini?

Mtumba Man akiwa kwenye mahojiano alisimulia jinsi alitaka kuitoa uhai baada ya kuwa maarufu, kwani atu walikuwa wanaona ana pesa ila hana.

Hata baada ya kuwa maarufu, Sande alisema kwamba yuko maarufu nchini ilhali hana pesa.

"Ushawahi kuwa maarufu au mashuhuri ila huna pesa, mama yako anaona hutaki kumsaidia na una pesa dada yako anaona tu hivyo, watu nyumbani wanajua na kufahamu uko na pesa kwa sababu wewe ni mtu mashuhuri, juzi karibu nijitoe uhai, ni ngumu kuwa mashuhuri lakini huna pesa

Kuuza mitumba kumebadilisha maisha yangu ata kabla sijafahamika sana nchini."

Huku akizungumzia changamoto za kazi yake alidai kwamba watu wengi wamekuwa wakimuita shoga ilhali yeye sio shoga.