Diamond aacha wengi na gumzo baada ya kufichua kuwa vito vyake vya mkono mmoja viligharimu Milioni 27

Muhtasari
  • Mwimbaji wa Tanzania Diamond amewaacha wengi gumzo baada ya kufichua kiasi cha pesa kinachostahili vito vyake vya mkono mmoja
Diamond Platnumz
Image: Hisani

Mwimbaji wa Tanzania Diamond amewaacha wengi gumzo baada ya kufichua kiasi cha pesa kinachostahili vito vyake vya mkono mmoja.

Mwimbaji huyo aliweka vito hivi kwenye akaunti yake ya Instagram abd alisema kiasi cha pesa wanachogharimu.

Amethibitisha mara moja ya kutosha kwamba yeye ni tajiri na bado anapata pesa nzuri kutoka kwa muziki na biashara zake.

Moja ya chapisho alionyesha kuwa pete kwenye vidole vyake zinastahili dola 100,000. Kubadilisha hizo kuwa pesa za Kenya, ambazo zingekuwa sawa 10,000,000.

Hiki ni kiasi cha pesa ambacho kinaweza kulipa mishahara ya kimsingi ya wafanyikazi wengi.

Diamond Platinumz ni mfano mwema kwa wengi kwa sababu,  alianza usanii wake kwa unyenyekevu nakuendeleza maisha yake kwa uvumilivu na kujitolea.

Sasa, yeye ni mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa nchini Tanzania na Afrika Mashariki.

Mapema, alionyesha mapambo yake ya mkono ambayo inaonekana kuwa ya almasi na madai ya kwamba vidole vyake vilikuwa na thamani ya dola 100k wakati mkono wote ulikuwa na thamani ya dola 177k ambayo ni sawa na Ksh 19,894,800.

Diamond ambaye pia anajulikana kama Simba alisemekana kuwa na thamani ya dola milioni 5 tu. Hiyo ni kulingana na ripoti ya gazeti la Forbes ambayo ilitolewa mapema mwaka huu.