Hata haumiliki baiskeli,'KRG achukua gari alilomzawadi aliyekuwa mkewe

Muhtasari
  • Katika video aliopakia kwenye ukuraa wkee wa instagram, KRG alifichua kwamba amechukua gari ambalo alikuwa amemzawadi hivi juzi huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa
  • Haya yanajiri kiezi 2 baada ya wawili hao kutengana, huku KRG akibaki na watoto wake wawili
KRG
Image: Hisani

Msanii chipukizi KRG the Don amemnyang'anya   mke wake wa zamani gari ambalo alikuwa amemzawadi.

Katika video aliopakia kwenye ukuraa wkee wa instagram, KRG alifichua kwamba amechukua gari ambalo alikuwa amemzawadi hivi juzi huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Haya yanajiri kiezi 2 baada ya wawili hao kutengana, huku KRG akibaki na watoto wake wawili.

Awali akiwa kwenye mahojiano KRG alisema kwamba mkewe hakumtambua pamoja na wanawe, ila alitambua  familia yake na ndugu zake.

"Mwanamke ni kama nguzo ya familia na akipotea haya basi familia inatawanyika, lakini kila mtu anamaamuzi yake lakini mimi na watoto wangu tushaazoea

Watoto wangu wanajua kila kitu,lakini tuache hayo kwa maana ana maisha yake na mimi nina maisha yangu

Kiini kikubwa cha ndoa yangu kuvunjika aliwasikiza watu wa nje, hatutambua mimi na watoto wangu  kama familia yake aliamini upande wao na kuwasikiza

Uhusiano wangu na Mungu ni mzuri, kwa maana Mungu huwa anakuja kwanza familia alafu pesa," Alisema KRG.

Pia msanii huyo alisema kwamba hajawahi mdanganya mke wake, kwani akiwa kwenye uhusiano na mwanamke mwingine alikuwa ameshaamwambia.

Aidha alifichua ana watoto 4 na baby mama 3.

Kabla ya kuchukua gari hiyo msanii huyo alimkejeli mkewe, na kusema kwamba hamiliki hata baiskeli kwa bivyo hapaswi kujisifu na gari ambalo sio lake.

"Watu wanene watasalia kuwa wanene, watu wa wera watolewe wapo elfu 350, hata shilingi moja huwezi pata acha elfu 350

Eti gari langu na hata haumili baiskeli," Alisema KRG.