Diamond Platinumz, Nandy, Sauti Sol na Wizkid wang'aa katika tuzo za Afrimma

Muhtasari
  • Wawili hao waliibuka washindi katika orodha za Mwanamuziki bora wa kiume na yule wa kike Afrika mashariki
Diamond Platnumz
Image: Hisani

Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platinumz na Nandy kutoka Tanzania wameibuka washindi katika tuzo za Afrimma Awards 2021.

Wawili hao waliibuka washindi katika orodha za Mwanamuziki bora wa kiume na yule wa kike Afrika mashariki.

Diamond Platinumz aliibuka mshindi baada ya kumshinda Ali Kiba aliyeonekana kuwa mpinzani wake mkuu, Kaligraph Jones kutoka Kenya , Otile Brown kutoka Kenya, Msanii Meddy kutoka Rwanda, The Ben kutoka Rwanda na Eddy Kenzo kutoka Tanzania.

Vilevile video ya wimbo wa Flavour akishirikiana na Diamond Platinumz na fally Ipupa -Berna ilitawazwa kuwa video bora ya mwaka.

Aliwashinda Tay C - Le Temps, Teni - Hustle, Mz Vee - Baddest Boss, Zuchu - Sukari, Ray Vanny x ,Innos'B - Kelebe Rema - Bounce na Wizkid ft Tems - Essence

Upande wa wanawake Nandy aliweza kumshinda Zuchu aliyeonekana kuwa mshindani wake wa karibu , Nadia Mukami kutoka Kenya, aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Diamond Platinumz kutoka Kenya , Tanasha Donna kutoka Kenya, Nikita Kering kutoka Kenya, Vinka kutoka Uganda na Knowles Butera kutoka Rwanda.

Hatahivyo taji la mwanamuziki bora wa mwaka lilielekea Magharibi mwa Afrika huku Wizkid akiibuka mshindi. Wizkid aliwashinda Burnaboy na Fali Ipupa na kuchukua taji hilo.

Wengine ni pamoja na Aya Nakamura Mali, El Grande Toto kutoka Morocco , Tay C kutoka Cameroon na Dadju kutoka Congo.

Vilevile Wizkid alitangazwa kuwa mshindi wa wimbo bora wa mwaka kupitia wimbo wake alioshirikiana na Tems na Justin Bierber .

Katika Orodha hiyo ,mwanamuziki huyo maarufu Afrika, Ulaya na Marekani aliwashinda Focalistic x Davido - 'Ke Star' Remix, Ladipoe ft Buju - Feeling, Calema ft Perola , Soraia Ramos & Manecas Costa - Kua Buaru, Dj Tarico x Burna Boy - Yaba Buluku,Tay C - Le Temps, Naira Marley x Busiswa - Coming na Nviiri the Storyteller ft Bien - Niko Sawa.

Kundi la Sauti ndilo lililoshinda kundi bora la muziki Afrika, huku Mercy Chinwo akishinda orodha ya msanii bora wa nyimbo za Gospel , naye David akishinda wimbo wenye ushirikiano bora zaidi .