Mungu bado ananipenda,'Msanii Akothee asema baada ya kuhusika katika ajali

Muhtasari
  • Kulingana na msanii huyo hajui nini kilitendeka lakini licha ya yote Mungu anampenda
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Msanii maarufu Esther Akoth almaarufu Akothee kupitia ukurasa wake wa instagram amefichua kwamba mchana wa Jumatatu alihusika katika ajali.

Kulingana na msanii huyo hajui nini kilitendeka lakini licha ya yote Mungu anampenda.

Pia alipakia video akitibu majeraha aliyoyapata kwenye ajali hiyo.

"Natibu majeraha ambayo nimepata, Mungu bado ananipenda mguu ulieenda kwenye breki na kugonga uso wangu kwenye usukani na magoti yangu

Sasa najua kwa nini hupaswi kuendesha gari bila viatu," Aliandika Akothee.

Kwenye chapisho lingine Akothee aliandika;

"Nimeepuka kifo chupuchupu! bado anapata nafuu kutokana na mshtuko ๐Ÿ™๐Ÿ™ Sijui ni nini kilitokea ๐Ÿ™."