Najijua kwa kucheat-Diamond Platnumz atoa sababu kuu ya kutooa

Muhtasari
  • Katika kibao chake cha 'Nawaza' ,sanii huyo alizungumzia mambo kadha wa kadha ambayo yamekuwa yakizunguka maisha yake
Diamondplatnumz
Diamondplatnumz
Image: Instagram KWA HISANI

Staa wa bongo kutoka Tanzania Diamond Platnumz ametoa EP yake ambayo ilikuwa imesubiriwa sana mashabiki wake.

Katika kibao chake cha 'Nawaza' ,sanii huyo alizungumzia mambo kadha wa kadha ambayo yamekuwa yakizunguka maisha yake.

Katika kibao hicho Diamond amezungumzia jinsi ugomvi wake na Alikiba aliuona ni ushamba, kwani walikuwa wanapigania mashabiki.

Aidha msanii huyo amezungumzia kipi kitachomuua na iwapo lebo yake ya Wasafi itaendelea au itaisha baada yake kuaga dunia.

"Nawaza siku nikifa sijui wasafi itakufa nawaza sijui maradhi ama ajali itanikuta,nawaza nani mama Dangote nani chozi atamfuta

Nawaza sijui nyimbo zangu watazikumbuka," Diamond Alisema.

Staa huyo amekiri kwamba ananjijua kwa kuwadanganya wanawake, hivo basi ni jambo ambalo linamzuia kuoa.

"Nilowaza leonishawaza sana ninachoshindwa kuoa kipi, nikagundua naepusha lawama, maana najijua kwa kucheat