'Ni ubaguzi mkubwa,'Sonko azungumza baada ya kuzuiwa kuhudhuria sherehe za Madaraka

Muhtasari
  • Ameushutumu uongozi wa Mombasa kwa ufisadi ambao umesababisha viwango vya juu vya umaskini miongoni mwa wenyeji
Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko mnamo Machi 30
MIKE SONKO Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko mnamo Machi 30
Image: BRIAN OTIENO

Wakenya wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta leo wamekusanyika katika bustani ya Uhuru kusherehekea Sikukuu ya Madaraka.

Leo ni muhimu katika Historia ya Kenya kwani inaadhimisha siku ya 1963 ambapo Kenya ilijipatia utawala wa ndani kutoka kwa Serikali ya Kikoloni ya Uingereza.

Hafla hiyo pia inafanyika katika Kaunti zingine zote nchini Kenya zikiongozwa na Magavana wa Kaunti husika.

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Mike Sonko amelalamika kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii baada ya kunyimwa fursa ya kusherehekea Sikukuu ya Madaraka katika Kaunti ya Mombasa inayoongozwa na Gavana Hassan Joho.

Sonko amehoji ni kwa nini Serikali ya Kaunti ya Mombasa imeweka sharti kwa mtu yeyote anayehudhuria hafla hiyo kukosa kadi ya mwaliko ambayo umenyimwa ufikiaji.

Sonko amekosoa hatua ya Serikali ya Kaunti ya Mombasa huku akitoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati.

Ameushutumu uongozi wa Mombasa kwa ufisadi ambao umesababisha viwango vya juu vya umaskini miongoni mwa wenyeji.

"Rais Uhuru Kenyatta hebu ingilia hili swala. Yani kwenda kusherekea madaraka day na Wakenya wengine ati lazima uwe umealikwa na card

Hii ni ubaguzi mkubwa sana na ndio tunasema nilazima kuikomboa Mombasa kutoka kwa Minyororo za Umasikini na Uongozi duni ambao umenufaisha viongozi wanafik na watu binafsi ambao wanadhani hii Mombasa ni yao na kuacha Wana Mombasa wengi Kwenye umasikini. Mabadiliko lazima. Kuweni na siku njema,"Sonko Aliandika.