Sauti Sol waahirisha ziara ya Ulaya kufuatia kuchelewa kwa Visa

Muhtasari

•Bendi hiyo ilitarajiwa kuzuru maeneo kadhaa Ulaya baadae mwezi huu ili kutumbuiza wafuasi wao. 

•Baadhi ya maeneo ambayo walipanga kuzuru ni pamoja na Bristol, Leeds, Manchester na London.

Bendi ya Sauti Sol
Bendi ya Sauti Sol
Image: HISANI

Kwa mara ya pili bendi ya Sauti Sol imeahirisha ziara yao ya kimuziki katika bara Ulaya.

Bendi hiyo ilitarajiwa kuzuru maeneo kadhaa Ulaya baadae mwezi huu ili kutumbuiza wafuasi wao. 

Kupitia ukurasa wao wa Instagram, wanamuziki hao walisema wamelazimika kuahirisha ziara yao kutokana na kuchelewa kwa Visa ambako kumechangiwa na vita vya Ukraine.

‘Inasikitisha sana kwa mara nyingine sisi kukatiza safari yetu ya Ulaya, vitu zikikuwa sawa, tutatimiza ahadi yetu kwa mashabiki wetu’ Sauti Sol walisema.

Baadhi ya maeneo ambayo walipanga kuzuru ni pamoja na Bristol, Leeds, Manchester na London. Walitarajiwa kutumbuiza katika maeneo mbalimbali ya burudani yakiwemoThekla,Belgrave,Club Academy na Indigo O2.

Sauti Sol hata hivyo wamewahakikishia mashabiki wao kuwa wanafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa ziara hiyo imefanyika kama walivyopanga.

Walisema kuwa wanazungumza na mapromota wao kuhusu uahirishaji wa tamasha hizo na kuziweka wazi Juma lijalo.