Fanyeni kazi kwa bidii-Sarah Kabu awashauri wanawake wasiwategemee sponsors

Sarah aliwaomba wanawake kufanya kazi kwa bidii na kumudu mambo bora zaidi maishani bila kutegemea wanaume wazee

Muhtasari
  • "Ladies work hard sio lazima ufurahie vitu kama hivyo kupitia sponyo usiteseke kwa mapenzi. Nikiwatakia furaha zote ambazo upendo unazo." Aliongeza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bonfire Adventures Sarah Kabu amempongeza mwimbaji Akothee ambaye hivi majuzi alimtambulisha mpenzi wake mpya  na kuwapa changamoto wanawake wasio na waume kujifunza kutoka kwa mama wa watoto watano.

Sarah aliwaomba wanawake kufanya kazi kwa bidii na kumudu mambo bora zaidi maishani bila kutegemea wanaume wazee, maarufu kama "sponsors" kufadhili maisha yao.

"Single ladies, picha hii inakuhusu? Yaani @akotheekenya anapiga picha na mpenzi wake mpya  kwenye bustani yake," Sarah aliandika, akibainisha kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Akothee Safaris ni hadithi ya mafanikio aliyojitengenezea.

"Ladies work hard sio lazima ufurahie vitu kama hivyo kupitia sponyo usiteseke kwa mapenzi. Nikiwatakia furaha zote ambazo upendo unazo." Aliongeza.

Watu hao mashuhuri wanafurahia urafiki wa karibu na kusaidiana kama ilivyokuwa miezi michache iliyopita Sarah alipohudhuria albamu na uzinduzi wa kitabu cha Akothee.