Zari ajawa bashasha baada ya mpenziwe mdogo kumsherehekea kwa ujumbe mzuri

Zari alipenda ujumbe wa mpenzi huyo wake mdogo na akachukua fursa kumshukuru.

Muhtasari

•Shakib, 31, alimtambua mama huyo wa watoto watano  kwa jukumu lake la kuwatia moyo watu wengine na kumtaka kuendelea.

•Wawili hao walianza kuchumbiana mwaka jana na uhusiano wao umekosolewa sana haswa kutokana na tofauti zao kubwa za umri.

Zari na mpenzi wake Shakib
Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Mpenzi mdogo wa mwanasoshalaiti mashuhuri wa Uganda Zari Hassan, Shakib Cham Lutaaya alimsherehekea kwa ujumbe maalum mnamo Jumatano wakati ulimwengu wote ukiadhimisha siku ya wanawake duniani.

Shakib, 31, alimtambua mama huyo wa watoto watano  kwa jukumu lake la kuwatia moyo watu wengine na kumtaka kuendelea.

"Heri ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwako Mpenzi! Wewe ni msukumo kwa wengi, endelea na kazi nzuri," alimwandikia mpenziwe.

Shakib aliandika ujumbe huo mzuri chini ya chapisho la Zari akiwatakia wanawake wote duniani siku njema ya wanawake.

Zari alipenda ujumbe wa mpenzi huyo wake mdogo na akachukua fursa kumshukuru.

"Asante boo," alijibu.

Mpenzi huyo wa zamani wa staa wa bongo Diamond Platnumz amekuwa kwenye mahusiano na Shakib Lutaaya kwa miezi kadhaa sasa na wawili hao wamekuwa wakionyesha wazi jinsi wanavyofurahia kuwa pamoja.

Wawili hao walianza kuchumbiana katikati ya mwaka jana na uhusiano wao umekabiliwa na ukosoaji mwingi haswa kutokana na tofauti zao kubwa za umri. Zari ana miaka 42 huku Shakib akiwa mdogo kwa miaka 10 kuliko yeye.

Wapenzi hao walidaiwa kuenda njia tofauti mapema mwaka huu baada ya kutoonekana pamoja kwa kipindi kirefu kirefu kama ilivyokuwa hapo awali. Tetesi hizo zilienea zaidi mwishoni mwa mwezi Januari wakati raia hao wawili wa Uganda walipochapisha jumbe za kimafumbo kwenye mitandao ya kijamii.

Zari aliibua wasiwasi kuhusu mahusiano yake na Shakib baada ya kuchapisha nukuu ambayo ilielezea hatari ya uwongo miongoni mwa watu wako wa karibu.

Baadhi ya watu hawaelewi jinsi uwongo unaweza kuwa sumu. Uongo huambukiza na kulaani mahusiano yenye furaha hadi unahisi kuumwa na tumbo kwa kuwaamini tena,

Haijalishi ni kiasi gani unampenda mtu, wakati mwingine huwezi kujizuia kujisikia kama aliiba Faraja yako. Huna raha tena kwa sababu unakisia kila kitu. Sasa, kuwaamini sio kazi rahisi. Sasa inahitaji bidii na wakati mwingine hiyo inachosha ilisomeka nukuu hiyo ya Horacio Jones ambayo alichapisha kwenye Snapchat.

Wiki chache zilizopita hata hivyo, mwanasoshalaiti huyo hata hivyo alizika tetesi za kuvunjika kwa mahusiano yake baada ya kuchapisha video zake na Shakib wakifurahia nyakati za kimapenzi pamoja

Kwenye akaunti yake wa Snapchat, mzazi mwenza huyo wa staa wa Bongo Diamond Platnumz alichapisha video inayomuonyesha akimuaga Shakib ambaye alikuwa akielekea mahali pengine ambapo hawakuficha.

"Tuonane hivi karibuni. Nakupenda,"  alisikika akisema kwenye video hiyo.

Shakib vilevile alimhakikishia mama huyo wa watoto watano kuhusu mapenzi yake makubwa kwake na kumuaga kwaheri.

"Kwaheri mpenzi wangu. Nakupenda," alisema.

Wapenzi hao wawili pia walionekana wakikumbatiana na kubusu midomoni walipokuwa katika uwanja wa ndege.