"Watanzania ni watu hasi na duni!" Zari Hassan awashambulia mashemeji wake

"Wachana na walimwengu, wakosa akili. Najivunia mabadiliko yako dada," alimwambia Gigy.

Muhtasari

•Zari amemtaka Gigy Money kupuuza jumbe za chuki kutoka kwa baadhi ya Watanzania ambao wamekuwa wakimshambulia huku akiwataja kuwa watu duni.

•Zari alimhakikishia mwanasoshalaiti huyo mwenzake kwamba ujumbe wake ulikuwa wa pongezi wala sioo matusi.

Zari Hassan na Gigy Money
Image: INSTAGRAM

Aliyekuwa mke wa staa wa Bongo Diamond Platnumz, Zari Hassan ameendelea kumwonyesha upendo mkubwa mwanasoshalaiti wa Tanzania, Gigy Money licha ya kukabiliwa na ukosoaji mkubwa hapo awali.

Hivi majuzi, kulikuwa na maoni mengi hasi kwenye ukurasa wa Instagram wa Gigy Money baada ya kuchapisha screenshot ya ujumbe mrefu wa Zari akimpongeza kwa maendeleo yake mengi tangu alipopata umaarufu

Mwanasoshalaiti huyo kutoka nchi ya Uganda amemtaka Gigy Money kupuuza jumbe za chuki kutoka kwa baadhi ya Watanzania ambao wamekuwa wakimshambulia huku akiwataja kuwa watu duni.

"Watanzania ni watu hasi na watu duni. Ndio maana wanauona kuwa ujumbe mbaya," aliandika kwenye Instastori.

Zari alimhakikishia mwanasoshalaiti huyo mwenzake kuwa ujumbe ambao alikuwa amemtumia awali ulikuwa mzuri.

"Umejifanyia wema na wengine wetu tunajivunia wewe. Wachana na walimwengu, wakosa akili. Najivunia mabadiliko yako dada. Endelea dada," alimwambia.

Katika ujumbe wake kwa Gigy, Zari alimpongeza kwa maendeleo yake huku akiweka wazi kuwa ameweza kujiboresha. Mama huyo wa watoto watano alisema kwamba miaka ya hapo awali Gigy Money alikuwa mtu mchafu na mshamba ila sasa ameweza kujibadilisha na kuwa mtu wa kuheshimika. 

Umeniingia akilini leo, Yaani kipindi cha ujauzito wa Tiffah ulikuwa unaonekana mchafu, kana kwamba hukuoga. Sasa unaonekana kuwajibika zaidi na mwenye hadhi sana.  Drama nyingi zimepungua." 

Awali ulikuwa na drama chafu ya ghetto, sasa inaonekana unachagua drama yako kwa makini. Nilitaka tu kusema, kaa ukiwa na hadhi. Inaonekana vizuri kwako. Ninajivunia kuona dada akionekana na kufanya vizuri zaidi," aliandika.

Zari alimhakikishia mwanasoshalaiti huyo mwenzake kwamba ujumbe wake ulikuwa wa pongezi wala sioo matusi.

"Zari kasema nimekuwa msafi," Gigy Money alitangazia wafuasi wake kwenye Instastori zake na kuweka ujumbe huo.

Zari Hassan na Gigy Money
Image: INSTAGRAM