Britney Spears kuhusu talaka: 'Sikuweza kuvumilia maumivu tena'

Britney Spears amezungumza kwa mara ya kwanza tangu mumewe Sam Asghari atangaze kutengana kwao.

Muhtasari

•Bw Asghari, 29, alitaja "tofauti zisizoweza kusuluhishwa" katika ombi la talaka lililowasilishwa Los Angeles Jumatano.

•Wanandoa hao walichumbiana mnamo Septemba 2021 na walifunga ndoa katika sherehe ndogo Juni mwaka jana.

Image: BBC

Britney Spears amezungumza kwa mara ya kwanza tangu mumewe Sam Asghari atangaze kutengana kwao, akisema "hangeweza kuvumilia maumivu tena".

Bw Asghari, 29, alitaja "tofauti zisizoweza kusuluhishwa" katika ombi la talaka lililowasilishwa Los Angeles Jumatano.

Anaomba msaada wa wanandoa na malipo ya ada za kisheria kulipwa na Bi Spears, nyaraka zinasema. Bi Spears, 41, alisema "alishtuka kidogo" kwamba uhusiano wake wa miaka sita na Bw Asghari ulikuwa umefikia kikomo.

Akizungumzia kutengana kwao kwenye chapisho la Instagram, mwimbaji huyo aliandika: "Siko hapa kuelezea kwa nini kwa sababu ni ukweli kwamba hakuna mahusiano." "Nimekuwa nikijikaza kwa nguvu kwa muda mrefu sana na Instagram yangu inaweza kuonekana kuwa sawa lakini iko mbali na ukweli na nadhani sote tunajua hilo," aliongeza.

"Ningependa kuonesha hisia zangu na machozi juu ya jinsi ninavyohisi lakini kwa sababu fulani imenibidi kuficha udhaifu wangu."

Bw Asghari, mwigizaji wa asili ya Iran na Marekani, mwanmitindo na mkufunzi wa mazoezi ya viungo, alikutana na Bi Spears alipokuwa akirekodi video ya wimbo wake wa Slumber Party mwaka wa 2016.

Wanandoa hao walichumbiana mnamo Septemba 2021 na walifunga ndoa katika sherehe ndogo Juni mwaka jana.

Uvumi wa mapambano yao ya ndoa uliripotiwa katika magazeti ya Marekani mwaka huu. Wawili hao walikuwa wameonekana hivi karibuni bila pete zao za ndoa hadharani.

Katika chapisho lake kwenye Instagram, Bw Asghari alisema: “Baada ya miaka 6 ya upendo na kujitolea kwa kila mmoja mimi na mke wangu tumeamua kumaliza safari yetu pamoja.

"Tutabaki na upendo na heshima tuliyonayo kwa kila mmoja na ninamtakia kila la kheri." Aliongeza.