Jaymo ule msee na mkewae waeleza safari yao ya mapenzi

Safari hii ya mapenzi haikuwa ya moja kwa moja, kwani ilimbidi jaymo apitie vikwazo na kuwa na subira kabla ya kuushinda moyo wa Fortune.

Muhtasari
  • Kiini cha uhusiano wa Jaymo na Fortune ni maadili wanayothamini sana. Kuheshimiana kwao kunatokana na uhusiano wa kiroho, usafi na moyo, na uhusiano wa kifamilia.

Mchekeshaji na muunda maudhui Wilson Muranira anayefahamika zaidi kama Jaymo ule msee pamoja na mkewe Catherine Wakio Munene almarufu Catey Fortune wamegusa nyoyo za wengi si tu kwa uhusiano wao bali pia na maudhui ya wanandoa wanaowapenda.

Safari hii ya mapenzi haikuwa nyororo, kwani ilimbidi jaymo apitie vikwazo na kuwa na subira kabla ya kuuteka moyo wa Fortune.

Njia ya Jaymo ilikuwa na subira; hakuwa na haraka ya kuanzisha mahaba. Badala yake, alichagua kuweka msingi wa urafiki kwanza.

Fortune alifichua uvumilivu aliouonyesha Jaymo kabla ya kumpa nafasi. Jaymo alisimama kando yake katika mahusiano mawili ya awali, akithibitisha uaminifu wake na kujitolea kama rafiki kabla ya safari ya kimapenzi kuanza.

"Nilikuwa na mahusiano mengine mawili kabla hajaja, aliniona kupitia mahusiano mawili, tulikuwa marafiki wazuri tu, haikuwa kitu kiotomatiki", alisema Fortune.

Alipoulizwa kuhusu mabadiliko ya moyo wake kuelekea kwa Jaymo, Fortune alionyesha imani yake katika hatima, akisema kwamba hakuna kitu kinachoweza kuzuia kile kinachokusudiwa kuwa.

Kiini cha uhusiano wa Jaymo na Fortune ni maadili wanayothamini sana. Kuheshimiana kwao kunatokana na uhusiano wa kiroho, usafi na moyo, na uhusiano wa kifamilia.

Jaymo alihisi umuhimu wa maadili haya akisema kuwa, " Lazima ujue mtu ako na uhusiano na Mungu, lazima ujue kama mtu ni roho safi, lazima ujue kama mtu ako na uhusiano gani na familia yake".

Safari ya wanandoa hao sasa inajumuisha binti na mtoto wao wa kiume ambao hivi majuzi walisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya pili, kuashiria hatua nyingine muhimu katika maisha yao ya pamoja.

Kando na ubunifu wa maudhui, Jaymo amekuwa kwenye redio kwa muda mrefu katika redio ya homeboyz na sasa yuko Trace FM.

Fortune kwa upande mwingine amebobea katika uundaji wa maudhui ya kidijitali na vipengele katika video na mumewe.