Jaymo Ule Msee, Catey Fortune wapata mtoto wa 2 mwaka mmoja baada ya mtoto wa kwanza

Mwaka mmoja baada ya kupata mtoto wa kiume, safari hii wamebarikiwa na binti.

Muhtasari

• Mchekeshaji huyo aliweka wazi kwamba ni mtoto wa kike aliyezaliwa saa moja kasoro dakika tano asubuhi ya Jumatatu Aprili 17.

Jaymo Ule Msee na mpenzi wake Catey Fortune wabarikiwa na mtoto wa pili.
Jaymo Ule Msee na mpenzi wake Catey Fortune wabarikiwa na mtoto wa pili.
Image: Instagram

Mchekeshaji ambaye pia ni mtangazaji wa redio Jaymo Ule Msee na mpenzi wake Catey Fortune wametangaza kubarikiwa na mtoto wa pili miezi 13 tu baada ya kupata mtoto wa kwanza.

Ule Msee alitangaza habari hizi mpya kupitia ukurasa wake wa Instagram akimshukuru mke wake Fortune kwa kuendelea kumfanya baba mkubwa ‘mubaba’.

Mchekeshaji huyo aliweka wazi kwamba ni mtoto wa kike aliyezaliwa saa moja kasoro dakika tano asubuhi ya Jumatatu Aprili 17.

“6:55 AM 17:04:2023 ...Asante KaG kwa kuthibitisha Hali yangu ya Mubaba tena ️ Karibu Nyumbani Mama,” Jaymo Ule Msee alisema.

Ujumbe huo aliouandika ni sawia kama ule aliouandika mwana jana Machi baada ya Fortune kumzalia mtoto wake wa kwanza, akisema kuwa kipindi hicho ndio alifanywa kujihisi ni mubaba kamili, ila baada ya mtoto wa pili, alisema hali yake ya ‘ubaba’ inazidi kudhibitishwa.

"11:05 PM 3:3:2022...Asante KaG kwa kunifanya 'Mubaba Halisi' ...Karibu Nyumbani Prince MM," aliandika kipindi hicho.

Mashabiki wake walifurika kwenye ukurasa huo na kumhongera baadhi wakimtania kwamba aliamua kufanya suala la kuzaa watoto kuwa kama mbio za marathoni, kwani ni mwaka mmoja tu umepita tangu kuzaa mtoto wa kwanza.

“Hongera, kaende kaende,” mchekeshaji Blessed Njugush aliandika.

“Hongera mtu wangu, familia inazidi kuwa kubwa,” KRG the Don aliandika.

Ule Msee alikuwa kwenye timu ya mawasiliano ya kampeni za aliyekuwa mgombea wa urais kupitia tikiti ya chama cha Roots, wakili msomi George Wajackoyah.