Mambo yamechemka: Carol Katrue mpenzi wa Miracle Baby atangaza yuko 'single'

Wiki 2 zilizopita, Katrue alidokeza kuwa mjamzito tena, mwezi mmoja tu baada ya kuzaa mtoto wa kwanza na nyota wa "Wamlambezi wamnyonyez"

Muhtasari

• Miracle Baby hata hivyo ana watoto wengine wanne na wanawake tofauti.

• Katika mahojiano ya awali, msanii huyo aliwahi nukuliwa akisema kwamba ndoto yake ni kuwa na watoto 17.

Carol Katrue atangaza kuwa singo
Carol Katrue atangaza kuwa singo
Image: Instagram

Carol Katrue, mpenzi wa msanii wa gengetone Miracle Baby ametangaza kuwa yuko singo, siku chache tu baada ya kudokeza kuwa na mimba ya pili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Katrue aliandika maneno “niko single” na kuweka emoji za kulia, pasi na kutoa taarifa Zaidi kuhusu kilichojiri.

Haijulikani kama ni kiki ya mitandaoni anatafuta au ni kweli wameachana na Miracle Baby.

Hii inajiri wiki mbili tu baada ya Katrue kutangaza kwamba alikuwa na ujauzito wa pili tena, mwezi mmoja tu baada ya kujifungua mtoto.

Carol Katrue aliingia kwenye mitandao ya kijamii Jumamosi 18 na kutangaza habari hiyo, akichapisha kifaa cha kupima ujauzito kwenye hadithi zake za Instagram na nukuu: "Kuna moto mlimani."

Mpenzi wake Miracle Baby, kwa upande wake, aliweka kifaa hicho cha ujauzito na kuandika: “...ni wiki tatu tangu kuzaliwa kwa mtoto hii nayo imejitokeza,” akiendelea na kuongeza; "beb samahani."

Katrue ambaye pia ni msanii walikutana na Miracle Baby miaka michache iliyopita baada ya mambo kumwendea mrama Miracle Baby katika kundi la Sailors Gang ambao walikuwa wanatamba na vibao moto vya gengetone.

Miracle Baby na Katrue walishikana pamoja na kuanza kuimba nyimbo za Mugithi, ambapo wamejizolea ufanisi mkubwa, mbali na gengetone.

Wenzi hao walimkaribisha mtoto wao wa kwanza pamoja Februari, 18 2023. Miracle Baby hata hivyo ana watoto wengine wanne na wanawake tofauti.

Katika mahojiano yaliyopita, alisema: “Mmoja aliachwa mlangoni kwangu kwenye beseni kwa hivyo ilinibidi kumlea. Hata hivyo, tunafanana na ninashuku kuwa yeye ni wangu.”

Alipoulizwa kwa nini hawezi kutulia na mwanamke mmoja, alisema anataka kuwa na watoto 17 katika maisha yake na hakuna mwanamke mmoja anayeweza kukubali kuzaa na kuwalea wote.

"Hakuna mwanamke atakayekubali kuzaa watoto 17. Mama wa watoto wanajuana na wako kwenye mahusiano mazuri," alisema.