Siwezi mruhusu Miracle Baby aingie chumba cha kujifungua - Carol Katrue

Kwa sababu utafika wakati akiona niko na uchungu atakuwa anajawa na hisia - Katrue alieleza.

Muhtasari

• Katrue alisema kwamba walianza kuchumbiana na msanii huyo kitambo ila aliweka mambo wazi kipindi binti huyo ako kidato cha tatu.

Carol Katrue wakiwa na mpenzi wake Peter Miracle Baby
Carol Katrue wakiwa na mpenzi wake Peter Miracle Baby
Image: instagram

Aliyekuwa mwanamuziki wa gengetone amabye kwa sasa amezamia miziki ya Kikuyu aina ya Mugithi, Peter Miracle Baby na mpenziwe Carol Katrue hivi majuzi waliweka wazi kuhusu kutarajia mwanao wa kwanza.

Miracle Baby na Katrue waliungana pamoja na kuanza kuimba nyimbo za Mugithi pindi kundi la Gengetone la Sailors ambalo lilikuwa linaongozwa na Miracle Baby liliposambaratika.

Wapenzi hao wawili wamekwea ngazi zao katika tasnia ya Mugithi mpaka kuliwekea jina lao nguzo ya kudumu na sasa wanatarajia mtoto wao wa kwanza pamoja.

Licha ya kutangaza hivyo, bado kuna hatua moja ambayo inamsubiria Peter Miracle Baby, nayo ni kumsindikiza mkewe ndani ya chumba cha kina mama kujifungua.

Akizungumza na Mungai Eve, Carol Katrue alisema kuwa haoni kabisa akimruhusu Miracle Baby kumsindikiza hadi katika chumba kile katika kile alisema kwamba haoni kama ni wazo zuri.

 “Sioni ikiwa poa. Akuwe karibu tu na hiyo hospitali lakini nikiwa na huo uchungu ataona si poa kwa sababu utafika wakati akiona niko na uchungu atakuwa anajawa na hisia, na nikiona yeye ndio anafaa kunibembeleza na analemewa na hisia basi nitaichukuliwa kuwa pia mimi siko sawa, hiyo ya kuja ndani nikijifungua sioni kama ni sawa,” Carol Katrue alieleza.

Katrue alisema kwamba walianza kuchumbiana na msanii huyo kitambo ila aliweka mambo wazi kipindi binti huyo ako kidato cha tatu.