Mtu asiniulize kuhusu babangu, sikujizaa - Miracle Baby ajibu mzee anayedai ni babake

Amjuae baba ya mtoto ni mama so io swali si yangu kujibu - Miracle Baby

Muhtasari

• “Mimi ndio babake Miracle Baby anaitwa Willy Mpole nilimzalia hapa Mlango Kubwa,” mzee huyo alisema.

Miracle Baby ajibu mzee anayedai ni mwanawe
Miracle Baby ajibu mzee anayedai ni mwanawe
Image: Facebook

Jana mitandao ya kijamii nchini Kenya ilisambazwa na video ya mzee mmoja aliyejitokeza akidai kwamba ni babake msanii wa Mugithi  Peter Miracle Baby.

Mzee huyo alisema kwamab kijana huyo aliyeuwa kiongozi wa kundi la Gengetone Sailors Gang ni mtoto wake na kwa jina kamili anaitwa Willy Mpole. Alizidi kuelezea kwamab alimzaa katika maeneo ya Mathare sehemu inaitwa Mlango Kubwa.

“Mimi ndio babake Miracle Baby anaitwa Willy Mpole nilimzalia hapa Mlango Kubwa,” mzee huyo alisema.

Alimtaka msanii huyo kumkwamua kutoka kwa lindi la umaskini wa mtaa wa mabanda wa Mathare na kumweka katika maisha angalau yenye tija.

Baada ya video hiyo kusambazwa mitandaoni, msanii Miracle Baby hatimaye amefunguka kuhusu ishu nzima na ameonekana kuchukua mkondo wa Ommy Dimpozw a kukana kabisa kwamab hamjui huyo mzee.

Miracle Baby kupitia ukurasa wake wa Instagram alisema kwamba yeye hana uwezo wa kumtambua kama babake kwani ukweli ni kwamba anayejua baba ni mama pekee.

Niseme Nini mimi Willy Mpole na msee mwingine asiniulize kuhusu babangu tena kwani coz sikujizaa mimi na amjuae baba ya mtoto ni mama so io swali si yangu kujibu,” Miracle Baby alisema.

Watu wengi walionekana kumuunga mkono msanii huyo katika suala hilo kwa kusema kwamba kumekuwa na mripuko wa kina baba wanaowatelekeza watoto wao kisha baadae nyota zao ziking’aa baba hawa wanajitokeza wakitaka kuteleza kwa ganda la ndizi la watoto hao.

Sakata hili linajiri huku nchini Tanzania msanii Ommy Dimpoz akiwa katika mzozo mkali mitandaoni baada ya klipu kuibuka kwamba yeye na babake hawala kutoka sahani moja na mzee wake sasa anataka kutambulika kama babake licha ya kumtelekeza awali.