Maoni mseto baada ya Dennis Karari kuwashtua mashabiki wake na mtoto

Video hiyo iliashiria kurejea kwa Karari kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukosekana, jambo ambalo alihusisha na uhitaji wa kazi yake.

Muhtasari
  • Alitabasamu kwa upole mtoto aliyelala huku akirekebisha blanketi lake.
Dennis Karari
Image: Instagram

Mtaalam wa vipodozi Dennis Karari amewashangaza mashabiki baada ya kuonekana kufichua kuwa yeye ni baba mpya.

Kwenye TikTok yake, Karari alishiriki video ya kupendeza akiwa amembeba mtoto mchanga mikononi mwake.  Alipgwa picha akiwa amemshikililia mtoto huku akiwa ameketi kwenye gari . 

"Baba mtoi," aliandika kipande hicho akionyesha kuwa yeye ndiye baba wa mtoto.

Video hiyo iliashiria kurejea kwa Karari kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukosekana, jambo ambalo alihusisha na uhitaji wa kazi yake.

"Mimi ni msanii wa mapambo na inanihitaji wakati wangu wote," alijibu shabiki mmoja.

Video aliyochapisha ilizua hisia tofauti. Wengine wakishangaa alienda wapi huku wengine wakiuliza alimpataje mtoto kwa kuwa walikuwa wanajua alikuwa katika kikundi cha LGBTQ.

Haya hapa ni baadhi ya maoni kutoka kwa mtandao:

Jimmy 254: Udaku zingine ziambatane na evidence tafasali😂

Kerubo Omweri:What do you mean he gave birth

Mwende:Uko TikTok mambo inaenda mbio🤣😂..ni kama washafika 2025😅

Nyambuu art Princess: Confuuuuuuseee themCongratulations to him🥰

I am wanjii raw: This man disappeared from my fyp and he appears when he already a dad😂I missed a whole book not even a chapter 😭💔

Your girl nana: If confuse the crowd was a person!!✅