Jamaa shoga alia na kuvuruga harusi ya mumewe baada ya kugundua anaoa mwanamke (Video)

Kizaazaa kilishuhudiwa katika kanisa moja baada ya mwanamume shoga kuvuruga harusi akidai kwamba mwanamume aliyekuwa anafunga harusi na mrembo wake ni mpenzi wake.

Muhtasari

• Kulingana na ripoti, shoga huyo na mpenzi wake walikuwa wamechumbiana kwa zaidi ya miaka 5 na kutupwa kwa mwanamke mwingine.

Mwanamume shoga avuruga harusi ya mpenziwe
Mwanamume shoga avuruga harusi ya mpenziwe
Image: Screengrab

Kizaazaa kilishuhudiwa katika kanisa moja nchini Afrika Kusini baada ya mwanamume shoga kuvuruga harusi akidai kwamba mwanamume aliyekuwa anafunga harusi na mrembo wake ni mpenzi wake.

Katika video fupi kutoka kwa tukio hilo, mwanamume huyo shoga alifika wakati mwafaka kabla ya mhubiri kuwashikanisha mke na mume kuwa kitu kimoja na kuzua rabsha, asiweze kutulizwa na mtu yeyote.

Jamaa huyo aliyekula na kusitunya alionekana akijitupa sakafuni na kujigaragaza kwa hasira akiteta kwamba mpenzi wake – mwanamume – alikuwa ameratibu harusi yake kinyemela licha ya kujua kwamba walikuwa katika uhusiano wa kishoga.

Kulingana na ripoti, shoga huyo na mpenzi wake walikuwa wamechumbiana kwa zaidi ya miaka 5 na kutupwa kwa mwanamke mwingine.

Licha ya mashuhuda wa tukio hilo kujaribu kumtuliza, bado alipiga kelele na kuapa kuharibu tukio zima.

Tazama video hapa chini kujua zaidi...