Nuru Okanga ashambuliwa na kashfa ya ushoga kisa picha na mzungu 'aliyekuja kumuona'

Hata hivyo Okanga alijitetea vikali kwa kusema kwamba mzungu huyo ni shabiki wake tu ambaye alisafiri kutoka Uholanzi kwa lengo moja tu - kumuona.

Muhtasari

• Licha ya kuweka wazi kwamba mzungu huyo ni shabiki wake aliyekuja kumuona tu, wanamitandao walimgeuzia Okanga mtutu wa maneno ya kashfa wakimtaka kunyoosha maelezo vizuri.

Nuru Okanga na mzungu shabiki yake.
Nuru Okanga na mzungu shabiki yake.
Image: Facebook

Mtetezi mkali wa sera za kinara wa Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga, Nuru Okanga amewashangaza mashabiki wake wengi baada ya kudai kwamba shabiki wake ngangari kutoka Uholanzi alifanya ziara nchini Kenya hivi majuzi kwa ajili ya kuja tu kumuona.

Okanga alipakia picha ya pamoja na shabiki huyo mzungu kutoka Uholanzi na kusema kwamba kilichomleta nchini si kingine Zaidi ya kuonana na Okanga tu.

“Kutana na shabiki wangu mzungu kutoka Uholanzi ambaye alisafiri kuja humu nchini kwa ajili ya kuniona tu,” Okanga aliambatanisha maandishi haya kwenye picha hiyo.

Licha ya kuweka wazi kwamba mzungu huyo ni shabiki wake aliyekuja kumuona tu, wanamitandao walimgeuzia Okanga mtutu wa maneno ya kashfa wakimtaka kunyoosha maelezo vizuri.

Kwa kupitia katika kipengele cha maoni kwenye picha hiyo, wengi walimbatiza na kashfa ya ushoga na mzungu huyo huku wengine wakimtukana kwamba anakubali kuja kuonwa na mzungu kama yeye ni mnyama pori.

Haya hapa ni baadhi ya maoni kutoka kwa mashabiki wake;

“Mh Nuru Maloba Okanga kukuona kwani wewe ni nyani kwenye mbuga ya wanyama?” anayejiita Yesu wa Tongaren alimuuliza.

“Unashika aje mwanaume Ivo sasa  ama unakuanga sim 2 “ oliver Kasigane Ngusale alisema.

“Huu ni ushoga” Fabby Fabbiano KE alisema.

“Okanga chungana na wazungu hawa ukonora watu yani atoke holland kuja kuona boy” Prince Kevo alimtahadharisha.

“Huyo ni Dem yako sisi sio wajinga” Charles Dickens alimwambia.

“Chunga sana, mabwana wanajipata mabibi currently ” John Edward KE.