Size 8 afichua kuwa amekuwa akifua nguo za ndani za mumewe kwa miaka 10 sasa!

Kumekuwa na maoni tofauti kutoka kwa Wakenya baada ya mwanamuziki Linet Munyali almaarufu Size 8 kusema kwamba amekuwa akifua nguo za mumewe za ndani, Dj Mo kwa miaka 10 iliyopita.

Muhtasari
  • “Mbona watu wanashangaa kusikia naoshewa nguo za ndani? Kwani nyinyi hamuoshewi?" Dj Mo aliuliza.
Dj. Mo Na Size 8

Kumekuwa na maoni tofauti kutoka kwa Wakenya baada ya mwanamuziki Linet Munyali almaarufu Size 8 kusema kwamba amekuwa akifua nguo za mumewe za ndani, Dj Mo  kwa miaka 10 iliyopita.

Wakati wa mazungumzo na mwimbaji wa nyimbo za injili Mesh Mpendwa na mkewe, Wapendwa Muziki, Size 8 na DJ Mo walishiriki kuhusu uhusiano wao, wakiwapa vidokezo vya ndoa yenye furaha.

"Tangu tufunge ndoa, Samuel Muraya almaarufu Dj Mo hajawahi kuosha nguo zake za ndani," alisema.

DJ Mo katika majibu yake alimtambua mkewe kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiifanya na kuwauliza wanaume wenzake kwanini zao hazioshwi na wake wao.

“Mbona watu wanashangaa kusikia naoshewa nguo za ndani? Kwani nyinyi hamuosheangwi?" Dj Mo aliuliza.

"Lazima nifanye kitu kumkumbusha yeye ndiye mkubwa wa familia yetu," Size 8 aliongeza.

Haya yote yalileta maoni tofauti tofauti kutoka kwa Wakenya. Haya ni baadhi ya maoni kutoka kwa Wakenya:

Wanza 001: Washing someone's boxers to remind him who he is? Make it make sense

its Anyango: Kwani who doesn't jameni😂😂😂

Empress Amani: Honestly there are some stuff I’d NEVER do for my partner; since when did we start discussing our “private” marital issues online? Anyways boundaries are so important to avoid being used badly 💯.

Esther Kavindu: To boost his self esteem ndio iko shida. Yaani you need your boxers washed to get your esteem in a relationship? Messed up

Etdeh Queen: I love size 8 ❤️

Marlenia Diketo: Not a big deal tunaoshea waume zetu boxers na sio eti ni kulazimishwa😅

Hawwaz: 🤣🤣🤣🤣okay

Balque: Good wife

Eddy Gitonga: Not a problem

Lucy Mutiso: "A way to remind him who he is" what does that mean?