Sonko amuokoa Kibe kutoka kwa umati wa vijana wenye hasira

Vijana waliojawa na hasira walivamia mkahawa ambamo Kibe alikuwa akifanya mahojiano ya moja kwa moja kwenye TikTok na Sonko.

Muhtasari
  • Katika video, gavana huyo wa zamani anaonekana akiwashawishi vijana hao warudi nyuma, akiwasindikiza nje ya klabu.
Image: HISANI

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko alimuokoa mwanablogu Andrew Kibe kutoka kwa umati wa watu jijini Nairobi kwenye Barabara ya Ngong.

Haya yalijiri baada ya vijana hao waliojawa na hasira kuvamia  mkahawa alimokuwa  ambapo Kibe alikuwa akifanya  mahojiano ya moja kwa moja kwenye TikTok na gavana huyo wa zamani mnamo Aprili 29.

Vijana hao walivamia klabu hicho huku wakitaka Kibe atolewe eneo hilo.

Vijana hao waliosema walijua kuhusu mahojiano hayo kutoka kwa akaunti za Kibe za mitandao ya kijamii walilazimika kurudi nyuma baada ya Sonko kuwashawishi waondoke kwenye eneo la tukio.

Wakati wa mahojiano, Sonko, ambaye anajulikana kwa maisha yake ya kifahari alisema kuwa kwa sasa hana kazi na amekuwa na wasifu wa chini.

Katika video, gavana huyo wa zamani anaonekana akiwashawishi vijana hao warudi nyuma, akiwasindikiza nje ya klabu.

Wakati kisa hicho kikiendelea, Kibe anaonekana ameketi kwa utulivu, akitazama hali ilivyo huku umati wa watu ukiwa umezuiwa na usalama wa Sonko.

Haijabainika jinsi Sonko na Kibe walikubali kukutana kwa mahojiano baada ya kuwa na uhusiano mbaya tangu mwaka jana.

Mwaka jana, Sonko na Kibe walihusika katika ugomvi kwenye mitandao ya kijamii baada ya gavana huyo wa zamani kumtaka Kibe ajizuie kutaja jina lake kwenye kipindi chake cha YouTube na kuingilia maisha yake ya kibinafsi.

Pia, Sonko alionyesha kufadhaishwa na madai ya Kibe kuwashambulia watu mashuhuri wa Kenya, haswa wanawake.

“Nimekusikia. Mimi sio mjinga. Acha maisha yangu ya kibinafsi. Mimi ni chapa kwangu. Sihitaji kuionyesha. Acha kushambulia wanawake,” Sonko alisema mwaka jana.