Zari Hassan afunguka kuhusu anachofurahia zaidi kuhusu ziara za nyumbani, Uganda

"Maisha ya diaspora sio mazuri kila wakati," alisema.

Muhtasari

•Zari alizungumza kuhusu jinsi anavyopenda kuwa katika nchi yake kwani huwa anapata nafasi za kuhudhuria harusi.

•Alibainisha kuwa tofauti na akiwa nchini Uganda, kwa kawaida huwa hahudhurii harusi wakati akiwa Afrika Kusini.

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Mwanasosholaiti maarufu wa Uganda Zari Hassan amelinganisha maisha katika nchi yake ya kuzaliwa Uganda, na maisha akiwa nje ya nchi , Afrika Kusini, ambako ndiko anakoishi kwa sasa.

Katika chapisho la siku ya Jumapili, mama huyo wa watoto watano alizungumza kuhusu jinsi anavyopenda kuwa katika nchi yake kwani huwa anapata nafasi za kuhudhuria harusi.

Alibainisha kuwa tofauti na akiwa nchini Uganda, kwa kawaida huwa hahudhurii harusi wakati akiwa Afrika Kusini ambako amekuwa katika miaka michache iliyopita.

"Sehemu nzuri ya kurudi nyumbani (Uganda) ni kuhudhuria harusi, kitu ambacho sifanyi nikiwa Afrika Kusini," Zari alisema kupitia mtandao wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe wake na picha nzuri zake na mumewe Shakib Cham Lutaaya wakifurahia nyakati za kimapenzi wakati wa ziara yao ya hivi majuzi nchini Uganda ambapo walihudhuria harusi.

"Maisha ya diaspora sio mazuri kila wakati," alisema.

Mumewe, Shakib alionekana pia kufurahia wakati huo na alitumia fursa hiyo kuzungumza kuhusu jinsi anavyojisikia vizuri akiwa na mama huyo wa watoto watano.

"Na wewe kila wakati ni maalum," alisema.

Wanandoa hao, ambao wote ni Waganda, hivi majuzi walitembelea nchi jirani ambapo walifurahia na kuhudhuria harusi pamoja.

Zari na Shakib walirasimisha ndoa yao katika harusi ya faragha iliyofanyika nchini Afrika Kusini mapema mwezi uliopita. Wawili hao wamekuwa wakichumbiana kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Maelezo ya harusi hiyo yalikuwa yamefichwa sana lakini tulifanikiwa kupata baadhi ya picha na video za sherehe hiyo ya kukata na shoka.

Wawili hao walihalalisha muungano wao wa muda mrefu kwa mara ya kwanza katika harusi ya kidini ya Kiislamu (Nikah) mapema mwaka jana.