
MJASIRIAMALI Esther Akothee ameonyesha kughafilika kwake baada ya mwanamke mmoja aliyemsaidia takribani wiki moja iliyopita kurudi kwake tena akihitaji msaada zaidi.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook,
Akothee alichapisha ujumbe huo akisema kwamba siku 4 zilizopita, mwanamke huyo
alimlilia kwamba hakuwa na mahali pa kulala baada ya kufungiwa nyumba.
Alimlilia msanii huyo ambaye kwa utu
aliguswa na kumlipia kodi ya kila mwezi ya shilingi elfu 6.
Hata hivyo, kilichompandisha mori
Akothee ni baada ya mwanamke huyo kurudi kwake tena safari hii akiwa na hitaji
jipya la kutaka msaada wa hela za kununua chakula.
Ni suala lililoonekana kumkera Akothee
ambaye alilichapisha kwenye Facebook yake na kuvutia maoni mseto, baadhi
wakihisi mwanamke huyo aliyesaidiwa alikwenda hatua zaidi ya kuwa na mazoea.
“Unakumbuka yule mama fua nilimtumia 6k
siku 4 zilizopita kumlipia malimbikizo ya nyumba yake? Alipiga simu jana kuomba
pesa tena akisema anahitaji msaada wangu na hana hata 50 bob kumudu mahali pa
kulala. "Boss ni mimi petronila, tafadhali mum, Leo sina magali pa Kulala,
nitumie kitu kidogo nijisaidie1" Akothee alisema.
Katika hali ya kushangaza, Akothee Alifichua
kwamba mwanamke huyo hata hakuweza kulipa kodi hiyo na kumtaja kama mama mwenye
umri wa miambaye ni mvivu kupindukia.
“Hajawahi kulipa kodi alisema mwenye
nyumba hakuwahi kupokea simu zake 🙏Kwa hivyo niliachana na
vita kwa sababu nimeshindwa, yeye ni mvivu hata kutunza kwa muda mrefu,
anaficha nguo chafu na huwa na haraka ya kuondoka, hawezi kupika wala kusafisha
nyumba vizuri, hadithi zake zote hazijumuishi yeye ni marehemu 50s 🙏 Mungu tafadhali, sitaki kuwa yeye nikua niache nibaki
mitaani. Na hii uwomgo wa ujinga haha
upate billionaire, huwezi kujenga punje inaishia hapo,” alisema.