Aliyekuwa muigizaji wa Machachari Stella atupilia mbali madai kuwa ni msagaji na ana msongo wa mawazo

Muhtasari
  • Muigizaji Stella akana madai kwamba yeye ni msagaji na ana msongo wa mawazo
  • Pia muigizaji huyo alisema kwamba hatumii dawa za kulevya
  • Hii ni baada ya video kuenea na madai hayo
Stella Machachari
Stella Machachari

Muigizaji Natasha Ngagie almaarufu Stella, aliyekuwa anaigiza katika kipindi cha Machachari kupitia kwenye ukurasa wake w instagram ametupilia mbali na kukana madai kwamba yeye ni msagaji ana msongo wa mawazo na pia anatumia dawa za kulevya.

Umaarufu wa uigizaji wake ulionekana tangu alipokuwa mtoto mchanga huku akiingiza kwenye kipindi cha Machachari kilichokuwa kina peperushwa kupitia kwa runinga ya Citizen.

Tangu Stella kuacha kuonekana kwenye runinga madai tofauti yamekuwa yakienea kwenye mitandao ya kijamii.

 

Huku akikana madai hayo aliwasihi wanablogu kutoandika habari kwa ajili ya kuwapendeza mashabiki wao.

Video imekuwa ikienea kwenye mitandao ya youtube na kudai kwamba muigizaji huyo ni msagaji.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, Stella alikana madai hayo na kusema ni ya uongo.

"Video imekuwa ikienea sana kwenye mitandao ya youtube na madai kusambazwa kuwa natumia dawa za kulevya, mimi ni msagaji na kwamba nina msongo wa mawazo na mambo mengine mengi

Niko hapa kuweka mambo wazi kwamba hayo si kweli, kwa maana siko kwenye runinga zeni haina maana kwamba nina mawazo

Wanablogu tafadhali wacheni kuandika habari kwa ajili ni habari tu."Stella Aliandika.