(+Picha) Mpenziwe Jowie Irungu Eleanor adai wameachana

Muhtasari
  • Mpenziye Jowie asema uhusiano wao umekwisha, huku akifichua kwamba alidanganya kuwa ni mkewe Jowie
  • Eleanor ambaye pia alikuwa meneja wa Jowie alisema anamtakia Jowie maisha marefu na hangetaka afuatilie kila aendako wala kwa kila jambo analofanya
117907586_935670980263257_6583431728613957532_n
117907586_935670980263257_6583431728613957532_n

Aliyekuwa mpenziye Jowie Irungu Eleanor Musangi,kupita kwenye ukurasa wake mwanablogu Edgar Obare amethibitisha na kudai kwamba wameachana na Jowie.

Ufichuzi huu umewashtua mashabiki wengi mitandaoni kwani wawili hao walikuwa wamethibitisha kwamba walikuwa wameoana pindi tu Jowie alipowachiliwa huru kwa dhamana ya KSh 2 milioni. 

Jowie anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani ambaye alipatikana akiwa ameuawa kinyama nyumbani kwake mtaani Kilimani mwaka wa 2019.

Eleanor ambaye pia alikuwa meneja wa Jowie alisema anamtakia Jowie maisha marefu na hangetaka afuatilie kila aendako wala kwa kila jambo analofanya.

" Kwa ajili ya sababu halali, nilikubali kuishi na Jowie mjini Nairobi kwa sababu polisi waliokuwa wakifuatilia kesi yake walitaka kujua anaishi na nani , nilimsaidia Jowie na moyo wangu wote, hali nilimpata singekubali ateseke," Eleanor alisema. 

Eleanor alisema ingawa hatua hiyo ilihatarisha taaluma yake ya kuwa mwamamitindo kimataifa , alikuwa na sababu za kutosha kumsaidia Jowie ambaye kwa wakati huyo alikuwa na msongo wa mawazo.

Hizi hapa baadhi ya picha za mawasiliano ya Musangi na Edgar Obare alizopakia kwenye mitandao ya kijamii ya instagram.