Mume wangu alikuwa amemuoa binamu yangu-Mwanamke afichua haya

Muhtasari
  • Mwanamke aeleza jinsi alifahamu mume wake alikuwa mume wa binamu yake
sad woman
sad woman

Kila kuchao tunazidi kushuhudia maajabu, huku wengi wakiamini kwamba ni siku za mwisho ambazo zimewadia.

Mwanamke wa miaka 22 alisimulia jnsi aligundua kwamba mume wake alikuwa, mume wa binamu yake.

Licha ya kuwa pamoja mwanamke huyo alikatalia na familia yao kwa ajili ya kitendo hicho, lakini hajaamua kuacha mumewe kwa ajili ya familia yake.

" Nilikuwa nasihi na ndugu yangu baada ya kumaliza kidato cha nne, alikuwa na tabia ya kuwaleta wanawake nyumbani, kisha nafua malazi ambayo walikuwa wanalalia, niliona ananibeba vibaya

Nilitoroka na nikaenda kwa mpenzi wangu, na kisha tukaanza maisha ya ndoa, baada ya muda mfupi nilifahamu kuwa alikuwa mume wa binamu yangu lakini walikuwa wameachana kwa mwaka mmoja

Familia yangu walinikataa na kuniambia kwamba mimi sio mtoto wao, na kama nataka kuwa mtoto wao niachana e na mume wangu, siko tayari kufuata masharti yao kwa maana nampenda mume wangu 

Niliwaoma msamaha wote lakini wamekataa kunisamehe, sijui sasa nifanye aje , kwa sababu siwezi achana na mume wangu," Alieleza mwanamke huyo.

Je ungekuwa mwanamke huyo ungefanya nini?