'Fanya bidii kuna watu wanatakuwa kama wewe,'Ushauri wake Snoop Dogg kwa msanii Diamond

Muhtasari
  • Rappa Snoop Dogg amshauri Diamond atie bidii katika kazi yake
Diamond Platnumz na Snoop Dogg
Image: Hisani

Baada ya staa wa bongo wa Diamond Platnumz baada ya kupoteza katika tuzo ya BET,hakuonyesha ulegevu wake bali amekuwa akishirikiana na wasanii wakutoka nchi mbalimbali kutoa vibao vipya.

Diamond ni miongoni mwa wasanii wa kupigiwa mfano Afrika mashariki, kwa bidii yake katika kazi yake.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amekuwa akipakia picha na rappa maarufu wa nchi ya marekani.

Hiyo ina maana kuwa msanii huyo wanaandaa kitu kwa mashabiki,je collabo yao itaweza ?

Siku ya jumatatu Diamond alipakia picha akiwa na rappa Sboop Dogg, ambaye anafahamika sana kwa umaarufu wake katika kazi yake.

Video ya rappa huyo akimsahuri msanii huyo jinsi ya kutia bidii katika kazi yake imeibuka.

Huu hapa ushauri wake kwa msanii Diamond.

"Wakati huu wakati hauangalii nambari, nilikuwa nikitazama nambari, kisha nikapepesa macho na kuanguka

Haupaswi kuanguka, kwa sababu kuna mtu mwingine atakayekuja, kama wewe ulivyokuja.

Utafanya kazi kwa bidii kwa sababu kuna watu wengine ambao wako nyuma yako, wanataka kuwa kama wewe hivi sas

Hiyo ndiyo unapaswa kujua. Unapoona mtu akiimba kama wewe, inafanana na wewe kwa sababu uko sahihi.

Katika mtaa wangu, kulikuwa na magenge ya kweli na wauzaji wa dawa za kulevya lakini wakati nilianza kuimba polepole waliweka dawa zao chini na kusema wanataka kuwa Mameneja, wazalishaji au kuwa kama mimi

Nilibadilisha mtazamo, sasa katika hood niggas yangu wanaishi vizuri. Kuimba ilikuwa baridi lakini haikuwa kwa kila mtu, ilikuwa mchezo wa Snoop Dogg.

Unakotokea, wewe ni msukumo wa kweli, Tanzania, Afrika, umebarikiwa," Alimwambia Snoop Dogg.

Diamond na Snoop Dogg walikutana kwenye studio na inaaminika kuwa wanafanya kazi kwenye wimbo ambao utapatikana kwenye Albamu mpya ya Platnumz.