'Kwa sasa niko single,'Msanii Juma Jux akiri

Muhtasari
  • Msanii kutoka Tanzania Juma Juxx anafahamika sana kwa ajili ya usanii wake, ambap amekuwa akitia bidii kila kuchao
  • JUma na Vanessa Mdee walichumbiana kwa muda lakini wakaachana, huku Vanessa akiendelea na maisha yake na hata kumchumbia msanii Rotimi

Msanii kutoka Tanzania Juma Juxx anafahamika sana kwa ajili ya usanii wake, ambap amekuwa akitia bidii kila kuchao.

JUma na Vanessa Mdee walichumbiana kwa muda lakini wakaachana, huku Vanessa akiendelea na maisha yake na hata kumchumbia msanii Rotimi.

Akiwa kwenye kipindi cha Wema Sepetu Juxx alidai kwamba kwa sasa hana mpenzi, na siku ambayo alitamani angekuwa na mpenzi ni siku ya wapendanao mwaka huu, kwani asilimia kubwa ya marafki zake walikuwa wakiwanunulia wapenzi wao zawadi ilhali yeye alikuwa 'single.'

Pia alizungumzia jinsi walichumbiana na aliyekuwa mpenzi wake kwa miaka 6 lakini uhusiano wao ulishindikana kwani walitengana.

"Kwa sasa niko single,miaka hiyo yote amekuwa msichana mzuri, miaka yote 6 nimekuwa nae tulifika sehemu ilibidi tutengane

Lakini zaidi ya yote tunaendelea vyema,wote tupo sawa,hakuna time nilitamani ningekuwa na mtu kama siku ya Valentines mwaka huu

Kwa sababu watu wangu wote wa karibu, walikuwa wananunua zawadi kwa watu wao," Alisema Juma Juxx.

Pia alisema kwamba huomba Mungu heri asiwe na mtoto kwani hayuko tayari kupata mtoto na mwanamke ambaye sio sahihi, na hiyo ndio sababu kuu ya kuchelewa kupata mtoto.