Ulikuwa celeb na mimi kinyangarika,'Mchekeshaji MCA Tricky amshukuru Eddie Butita huku akimpongeza

Muhtasari
  • Mchekeshaji MCA Tricky amshukuru Eddie Butita huku akimpongeza
  • Tricky  alisema alikuwa tu mtu ambaye hajulikani na watu na kwenye mitandao ya kijamii, ilhali Butita alikuwa anafahamika sana
butita
butita

Kwa mara ya wanza mchekeshaji wa kipindi cha Churchill MCA Tricky amefichua mtu ambaye alimfanya ajiunge na kipindi hicho.

KUlingana na Tricky, wakati alipokea simu ya Eddie Butita alikuwa ameanza kukata tamaa ya kujiunga na kipindi hicho.

Tricky  alisema alikuwa tu mtu ambaye hajulikani na watu na kwenye mitandao ya kijamii, ilhali Butita alikuwa anafahamika sana.

Huku akimpongeza kwa kujiunga na Netflix, Tricky alimshukuru Butita kwa kuwasaidia wachekeshaji.

"EDDIE BUTITA !! Baada ya ukaguzi wa onyesho la churchill (ukiwa part of creative team) Ulitafuta namba yangu na kuniita (kuja kesho)

Hata hivyo ni rahisi inaweza kuonekana kwako, juu ulikua celeb tayari na mimi kinyangarika fulani tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Haingekua hiyo simu hata labda ningeachana na onyesho la churchill, ambalo baadaye likawa hatua yangu ya kugeuza

 Vipindi vyote vikuu vya kuchekesha ambavyo tumewahi kuwa navyo katika 254 kutoka kwa wachekeshaji wetu vimepitia mikono yako, ni venye huwa hatukushukuruπŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£

Wakati umefika kwa Mungu kukuinua kwa ubunifu wako mkubwa na unyenyekevu. HONGERA BRO KWA KUWA MKURUGENZI WA KWANZA WA KIAFRIKA KWA SHOW ZA NETFLIX! πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘," Aliandika Tricky.