'Nitaeleza kila kitu,'Rappa KRG asema huku akidai atampa mkewe talaka

Muhtasari
  • Anasema kuwa ataelezea kila kitu kilichotokea katika ndoa yao tangu 2012 kwani amechoka na watu wanaomhukumu vibaya
Rappa KRG the Don
Image: INSTAGRAM/KRG

Mmoja wa rapa tajiri zaidi Kenya KRG the Don ametangaza kuwa kwa sasa anashughulikia jinsi atapata talaka kutoka kwa mkewe.

Msanii huyo alitoa tangazo hili kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii akidai kuwa atafichua yote yaliyotendeka kwenye ndoa yake.

Anasema kuwa ataelezea kila kitu kilichotokea katika ndoa yao tangu 2012 kwani amechoka na watu wanaomhukumu vibaya.

"Nitashughulikia maswala hivi karibuni na nitaelezea kila kitu kutoka 2012 hadi Tarehe ndio tukue kwenye ukurasa huo huo na watu ambao wananihukumu vibaya utakuwa na hadithi kamili bila kukamua chochote au kujaribu kugundua chochote nitaweka vitu kwa rangi nyeusi na nyeupe lakini kwa sasa niko sawa tu busy kwenye ukanda wa majaji kujaza talaka rasmi…," Aliandika KRG.

Jana rapa huyo alipakia picha ya mkewe ambapo alidai kwamba anampenda sana mkewe lakini alimwachisha kwa kuwasikiliza washauri ambao kulingana naye walitaka tu kuharibu maisha yake.

"Alikuwa mtu niliyempenda sana lakini alijiharibu kwa kuwasikiliza washauri wapumbavu ambao walitaka kuharibu maisha yake kwani alikuwa juu ya kila kitu kwa kila kitu bado alikuwa mdogo ………. Sawa Kweli sikio la kufa haliski dawa🙄🙄 anamchagua dada yake kuliko watoto wake mwenyewe."