Familia yangu hawanipendi tena-Vera Sidika adai

Muhtasari

Mwanasosholaiti Vera Sidika kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amedai kwamba upendo ambao alikuwa anapokea kutoka kwa marafiki na familia yake umemwendea mtoto wake

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasosholaiti Vera Sidika kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amedai kwamba upendo ambao alikuwa anapokea kutoka kwa marafiki na familia yake umemwendea mtoto wake.

Vera alitangaza kuwa na ujauzito wa msanii Brown Mauzo mapema mwaka huu, huku akijifungua mtoto wa kike  Oktoba.

Baada ya kujifungua Vera amekuwa akilalamika kwenye ukurasa wake wa instagram upendo aliokuwa anapokea unapewa mwanawe.

"Familia yangu na marafiki hawanipendi tena ninahisi kuachwa. Wanachojali ni Asia tu. Mapenzi yamebadilika. Huyu hakusema heri au habari za mchana. Alikwenda moja kwa moja kwenye biashara ya Asia. Dyna muthoni nitaanza kuwatoza shangazi wote wakaidi kwa picha," Aliandika Vera.

Mpenzi huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo alidai kwamba hakuhisi uchungu wowote alipofanyiwa upasuaji na hata baada ya kujifungua.

"Nilisema sijahisi uchungu wowote tangu nilipofanyiwa upasuaji hadi wa leo lakini watu hawaniamini kwa sababu wamezoea mbinu mzee za CS ambazo kila mtu aliogopa. Tena wanadhani eti sote tunaenda kwa daktari na hospitali moja kwa hivyo wanatarajia uhisi uchungu kama wa waliohisi" Vera amesema.