Shangazi yangu alimsaidia mumewe kuninyanyasa kingono-Asimulia Mwanamke

Muhtasari
  • Alianza kuishi na mjomba wake baada ya wazazi wake kuaga dunia, akiwa na umri wa miaka 14
sad woman
sad woman

Amewashangaza watu wengi mwanamke mmoja jijini Nairobi akisumulia jinsi mjomba wake alivyomshawishi kuavya mimba  baada ya kuwa katika uhusiano wa kisiri naye.

La kushangaza shangazi yake alikuwa anafahamu hayo yote, kwamba ananyanyaswa kingono, licha ya kuachiwa majukumu yote na wazazi wake.

Mwanamke huyo alitumia mitandao ya kijamii kusimulia masaibu yake  na kueleza jinsi shangazi  huyo alivyomtumia , kumpa mimba kisha akamwacha  hoi.

Alianza kuishi na mjomba wake baada ya wazazi wake kuaga dunia, akiwa na umri wa miaka 14.

"Nilipitia masiha magumu au wacha niseme jehonamu  nikiwa mikononi mwa shangazi yangu,badala ya kunilinda kama mtoto wake alimsaidia mume wake kuninyanyasa kingono kwa  muda mrefu sana

Ni maisha ambayo yanilinisababishia nipatwe na kiwewe hadi leo, nilikuwa jehanamu nikiwa duniani,pia shangazi yangu baada ya kugundua kwamba nina ujauzito wa mume wake alinishawashi niavye mimba hiyo mara moja

Nilitoroka sasa naishi maisha mazuri,kile nilijua ni kwamba Mungu akunyime kila kitu bali asiwa chukue wazazi wako mapema

Labda wazazi wangu wangekuwa hai singepitia mikononi mwa watu kama hao," Alisimualia mwanadada huyo.