Ujauzito upi huo haukuwi,'Msanii Nandy azungumzia madai ya kuwa mjamzito

Muhtasari
  • Akizungumza na wanahabari wa Tanzania, msanii huyo alisema kwamba atakapokuwa mjamzito, habari hizo hazitafichika kwa mashabiki wake

Msanii maarufu kutoka Tanzania Nandy amelazimika kuzungumzia madai kwamba anatarajia mtoto wake wa kwanza.

Akizungumza na wanahabari wa Tanzania, msanii huyo alisema kwamba atakapokuwa mjamzito, habari hizo hazitafichika kwa mashabiki wake.

“Kwa sasa hamna ujauzito, na mimi kama unafuatilia vizuri swala la uja uzito, huu ni mwaka wa pili sasa watu wanazungumzia. Nakumbuka nikifanya nyimbo ya Giza Kinene na nimeshiba zangu watu wanasema nina ujauzito.

Sasa Uja uzito gani huo ambao haukuwi, wala sizai? Watu waache kupredict vitu, na nikiwa na uja uzito hakuna kitu cha kuficha," Nandy alisema.

Miaka chache iliyopita Nandy akiwa kwenye mahojiano alidai kwamba kuna wakati alikuwa na ujauzito, bali akapoteza ujauzito wake.

Nandy ni miongoni mwa wasanii wa kike kutoka Tanzania ambao wameinuka kutoka kiwango kimoja hadi kingine, kutokana na bidii ya kazi yake.