Watu hawakuwa wananisikiza wakidhani mimi ni shoga-Shaniqwa asema

Muhtasari
  • Katika kipindi cha ilikuaje siku ya Jumatatu tulikuwa naye Kelvin Mwangi almaarufu Shaniqwa ambaye alifunguka kuhusu kazi yake na jinsi watu walimkejeli na kusema ni shoga
shaniqwa-5678
shaniqwa-5678

Katika kipindi cha ilikuaje siku ya Jumatatu tulikuwa naye Kelvin Mwangi almaarufu Shaniqwa ambaye alifunguka kuhusu kazi yake na jinsi watu walimkejeli na kusema ni shoga.

''Hapo awali, niliathirika. Ningetukanwa kwenye DM yangu, watu wana stress humu na wanakuachia lakini sasa watu wamezoea (tabia yangu.)

Kila mahali nilipoenda watu walidhani mimi ni shoga. Hawakutaka kusikiliza maelezo yangu kwamba nilikuwa naigiza. Ni watu tu waliokuwa karibu nami walioniamini. na nilikuwa sawa nayo, nilitamani sana kuwa celeb lakini mwenye hana mambo mengi

Nilipata kazi ya kuigiza kama msichana, nilipoitwa kuigiza kama Uhuru lakini ikashindikana," Alisema Shaniqwa.

HUku akizungumzia chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yake alisema kwamba alimpoteza mke wake na kazi kwa wakati mmoja.

Shaniqwa alipata umaarufu 2015 kutokana na lugha yake ya 'Ntakumurder'. Shaniqwa ni miongoni mwa watumbuizaji mashuhuri nchini Kenya ambao huvalia krosi wakati wa skits zao, licha ya kuwa wanyoofu.

Aliweka wazi kwamba yeye ni mwanamume na wala sio shoga, huku akisema anafahamu mkewe ameendelea na maisha yake.

"Ilifika mahali akaona kama mimi ni mzigo kwake, kosa kubwa nilifanya nikumwambia rafiki yangu amtafutie kazi, hapo ndipo nilimpoteza kabisa."

Hii hapa video ya mahojiano hayo;

Radio Jambo Kenya | Ongea Usikike | Ni kituo nambari moja Kenya kwa matangazo ya kiswahili. Vipindi vyake vina jumuisha Spoti,Mijadala moto moto na muziki wa Kiafrika #RadioJamboKenya Subscribe to RadioJambo Youtube - https://bit.ly/39wwc6u Mitandao ya Kijamii Instagram - https://rb.gy/e154d1 Facebook - https://rb.gy/09d1b9 Twitter - https://rb.gy/e23220