Makena Njeri sio rafiki yangu,'Brendah Jons azungumzia uhusiano wake na Makena

Muhtasari
  • Brendah Jones azungumzia uhusiano wake na Makena
Brendah Jons
Image: Brendah Jons/INSTAGRAM

Mmoja wa wabunifu wa maudhui nchini Kenya, Brendah Jons amejitokeza wazi kukanusha madai ambayo yaliibuka mtandaoni kwamba yeye ni rafiki wa karibu wa Makena Njeri.

Hii ni baada ya Makena kuachana na Mitchelle ambaye ni rafiki mkubwa wa Brendah, aliamua kuachana  na Makena.

Kulingana na Brendah, wanajuana tu kwenye mitandao ya kijamii, hii ni baada ya mmoja wa mashabiki wake  kwenye mitandao ya kijamii ya instagram kumuuliza iwapo yeye ni marafiki na Makena.

Brenda alisema kwamba anamfahamu Makena mtandaoni tu, lakini katika maisha halisi yeye si rafiki wa Makena Njeri.

"Kama unanifuata kwa ukaribu uanweza jua jinsi nahisi kuhusu jina 'rafiki'Mimi na Makena tunajuana tu mitandaoni lakini sio katika maisha ya kawaida kwa nini ulize lakini," Alijibu Brendah.

Aidha alisema kwamba hana mpango wa kupata mtoto, maishani mwake lakini mawazi hayo humjia mara kwa mara.